Ifahamu simu ya Samsung Galaxy S9 bei na Sifa zake


Simu mpya ya Samsung Galaxy S9, tayari imeshatoka rasmi ilizinduliwa kwenye mkutano wa MWC 2018 jijini Barcelona, Hispania. Ilizinduliwa pamoja na toleo jingine la, Samsung Galaxy S9 Plus. Simu ya inakuja na kamera iliyoboreshwa lakini ikiwa na vipengele sawa na ile ya zamani ya Samsung Galaxy S8. Samsung Galaxy S9 pia inamuonekana sawa na mtangulizi wake lakini ina uwezo zaidi wa mfumo wa AI. Kujiunga na mimi kama sisi kuhamisha makala kwenye smartphone hii moja kwa moja.

Kwa kuanza ningependa ujue kuwa simu hii mpya ya Samsung Galaxy S9 mwaka huu imetengenezwa maalum kwaajili ya watu wanaopenda picha yaani kifupi ni kuwa simu hii imefanyiwa maboresho makubwa sana kwenye upande wa kamera. kuliko sehemu nyingine.

Sifa za Samsung Galaxy S9

 • Mfumo wa Uendeshaji –  Android 8 (Oreo)
 • Ukubwa wa Kioo – 5.8-inch Quad HD + Curved Super AMOLED, 18.5:9 (529ppi)
 • Ukubwa wa Simu – Body: 147.7mm x 68.7mm x 8.5mm, 163g, IP68
 • Ukubwa wa Kamera – Kamera ya Nyuma Super Speed Dual Pixel 12MP AF sensor with OIS (F1.5/F2.4) Kamera ya Mbele 8MP AF (F1.7)
 • Ukubwa wa Processor – 10nm, 64-bit, Octa-core processor (2.8 GHz Quad + 1.7 GHz Quad)
 • Ukubwa wa RAM – 4GB RAM /
 • Ukubwa wa Ndani – 64GB + Micro SD Slot (up to 400 GB)
 • Ukubwa wa Battery – 3,000mAh yenye teknolojia ya Fast Wired Charging compatible with QC 2.0 / Fast Wireless Charging compatible with WPC and PMA
 • Uwezo wa Network – Enhanced 4X4 MIMO / CA, LAA, LTE Cat.18
 • Aina za Viunganishi –  Wi-Fi 802.11 a/b/g/n/ac (2.4/5GHz), VHT80 MU-MIMO, 1024QAM, Bluetooth® v 5.0 (LE up to 2Mbps), ANT+, USB type-C, NFC, Location (GPS, Galileo, Glonass, BeiDou)
 • Aina za Sensors – Iris sensor, Pressure sensor, Accelerometer, Barometer, Fingerprint sensor, Gyro sensor, Geomagnetic sensor, Hall sensor, HR sensor, Proximity sensor, RGB Light sensor
 • Aina ya Ulinzi – Authentication: Lock type: pattern, PIN, password, Biometric lock type: iris scanner, fingerprint scanner, face recognition, Intelligent Scan – biometric authentication with iris scanning and facial recognition
 • Mengine – Virtual Reality – Gear VR with Controller (SM-R325NZVAXAR), Google Daydream View

Muonekano na Kioo

Samsung Galaxy S9 ina muonekano unaofanana sana na mtangulizi wake. Pia imetengenezwa kwa mchanganyiko wa chuma na kioo ili kufanya simu iwe maridadi zaidi. Mabadiliko makubwa hapa ni uwepo wa fingerprint sensor . Bezel ya juu pia inaonekana kuwa nyembamba kidogo kuliko hapo awali na Samsung Galaxy S9 ina 3.5mm audio jack baadhi ya premium flagship za hivi karibuni zimeondoa mfumo huu ni jambo nzuri kuona wameiweka kwenye simu hii.Kitu kizuri kwenye simu ya Samsung Galaxy S9 ni ukubwa wa kioo chake cha 5.8-inch.

Betri na Kamera

Wengi wanapenda simu zenye betri yenye uwezo mkubwa lakini haipo hivyo kwenye simu ya Samsung Galaxy S9 kwani inakuja na betri yenye ujazo wa 3,000mAh. Hili ni tatizo tofauti na watangulizi wake ingawa ina tunza chaji kwa muda mrefu na pia ina uwezo wa kuchaji kwa haraka.

Tofauti na matoleo ya zamani, Samsung Galaxy S9 inakuka na uwezo mkubwa zaidi wa kupiga selfie kwani kamera yake ya mbele ina ukubwa wa 8MP. Kitu kingine kizuri kwenye simu hii ni Bixby Vision inayokupa uwezo wa kutafsiri maneno yaliyoandikwa kwa lugha nyingine kuwa katika lugha unayotaka wewe.

Vifaa na Programu

Samsung Galaxy S9 inakuja katika aina mbili tofauti inategemea na eneo ulilopo.Kwa Marekani na china simu hii inakuja na Octa-core Qualcom MSM8998 Snapdragon 845 processor pamoja na Adreno 630 GPU. Kwa maeneo ya EMEA (Ulaya, Uarabuni na Afrika) simu inakuja na Octa-core Exynos 9810 chipset pamoja na Mali-G72 MP18 GPU.

Samsung Galaxy S9 ina uwezo wa RAM wa 4GB ambao unatosha kuwezesha ufanyaji kazi bora wa simu yako.Pia unapata hifadhi ya ndani ya 64GB. Simu hii pia ina uwezo wa kutumia memori kadi hivyo unaweza kuongeza uhifadhi hadi kufikia 200GB. Samsung Galaxy S9 inatumia toleo la Android 8.0 Oreo pamoja na mfumo wa Samsung Experience UI.

Bei na Upatikanaji

Samsung Galaxy S9 kwa sasa inapatikana kwa pre-order lakini itaingizwa sokoni rasmi Marchi 16 kwa bei ya £739. Hii ni bei nafuu kuliko toleo la Samsung Galaxy S9 Plus.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA