Sambaza:

Itel S12 ni simu ya bei ndogo kutoka Itel kwa ajili ya wadau wa selfie – hasa, wale ambao hawana mahitaji mengi. Kama vile toleo la bei ya juu la Itel S32, kamera mbili za mbele na fingerprint scanner ni baadhi ya vipengele vya simu hii.
Itel S12

Sifa kuu na uwezo wa Itel S12

  • Kioo: Kioo inchi 5.0 ubora wa kioo ni 480 x 854 pixels
  • Prosesa: 1.3GHz quad-core Processor na RAM ya 1GB
  • Diski kuu: 8 GB pia unaweza kuweka memori kadi hadi ya GB 32
  • Kamera: Kamera mbili za mbele 2MP + 5MP , kamera ya nyuma ina MP 8
  • Mfumo wa uendeshaji: Android 7.0 (Nougat)
  • Mnara: 3G Data
  • Betri: Betri ina ujazo wa 2400 mAh
  • Usalama: Ina teknolojia ya fingerprint
SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Itel S32 na Itel S32 LTE bei na Sifa zake

Jinsi ilivyo na Kioo

Wengi wetu hawajui kuwa ITel ni kampuni inayozalisha vifaa ambavyo vinatia shaka katika ubunifu wake, hasa pale unapozingatia bei. Lakini inaonekana kufanya vizuri kidogo wakati huu, kwa kuongeza curves ili kufanya Itel S12 ikae vizuri unapoishika mkononi.

Itel S12 ina ukubwa wa kawaida wa  kioo inchi 5. Skrini ya kugusa ina uwezo wa pixels 480 x 854.

Kamera na Uhifadhi

Itel S12 ina kamera mbili upande wa mbele. Kamera moja ina 5MP na nyingine 2MP zinaboresha ubora wa selfies unazochukua.

Kamera ya nyuma ina 8MP ikiwa na mfumo wa autofocus, HDR na mifumo mingine. Uhifadhi wa ndani upo chini kwani ina GB 8. Unaweza kuongeza uhifadhi kwa kutumia kadi ya microSD ya hadi 32 GB.

Utendaji na OS

Prosesa ya quad-core 1.3GHz MediaTek imewekwa kusimamia ufanyaji kazi wa simu hii. Inapata msaada kutoka kwenye RAM ya GB 1 . Ni salama kusema usitarajie mambo mengi kwenye Itel S12 linapokuja swala ufanyaji kazi/utendaji.  Mfumo wa uendeshaji unaotumika ni Android 7.0 Nougat.

SOMA NA HII:  Nafasi za ajira serikalini sasa kuwafikia wahitimu kwa simu ya mkononi

Sifa Nyinginezo

Interestingly, the Itel S12 offers you a fingerprint sensor on its rear for added protection. This, perhaps, covers most of the other shortcomings.

Itel S12 ina betri ya ujazo wa 2,400mAh, sio mbaya sana ukilinganisha na uwezo mdogo wa skrini na chip inayotumika. Usitarajie kupata 4G LTE kwenye smartphone hii ya bei nafuu, lakini utapata uunganisho wa 3G.

Inashangaza, Itel S12 ina mfumo wa fingerprint kwa nyuma kuongeza usalama wa taarifa zako.

Bei na Upatikanaji

Itel S12 inapatikana Tanzania na Kenya pia. Unaweza kununua simu ya gharama nafuu ya Android katika maduka ya mtandaoni katika nchi yako. Bei ya Itel S12 nchini Tanzania  ni kuanzia Tsh 140000 – 200000

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako