Sambaza:

Infinix Note 4 Pro ni toleo la premium la Infinix Note 4. Kitu kipya zaidi kwenye simu hii ni kuwa imeongeza uwezo wa betri, ambapo itapelekea maisha marefu na bora ya betri. Infinix Note 4 Pro inapatikana katika muundo wa 32GB / 3GB tu na inakuja na Xpen Stylus (Kalamu ya kijanja) ambayo inaweza kufanya chaguzi za aina yake (smart select), kutumika kuandikia kwenye memo, sms, n.k.

Sifa kuu na uwezo wa Infinix Note 4 Pro

  • Aina ya kioo: IPS LCD
  • Kamera: Kamera ina MP 13 pamoja na flash 2, kamera ya nyuma ina MP 8
  • Laini za simu: Inakubali laini 2
  • Wembamba: 159.6 x 78.8 x 8.3mm (uzito ni gramu 200)
  • Mfumo wa uendeshaji: Android 7.0 (Nougat)
  • Mnara/Teknolojia nyinginezo: GPRS, Edge, 3G HSPA, 4G LTE, Bluetooth v4.0, Wi-Fi 802.11 b/g/n, hotspot, Micro USB na ina redio
  • Usalama: Ina teknolojia ya fingerprint iliyowekwa eneo la mbele.

Ukubwa, ubora wa kioo na Kamera

Infinix Note 4 Pro inafanana na Note 4 kimuonekano lakini inatoa chaguzi tofauti za rangi. Phablet inapatikana katika rangi za Kahawia, nyeusi, dhahabu na bluu.

SOMA NA HII:  Jinsi ya kuficha (hide) picha kwenye simu za android

Infinix Note 4 Pro ina kioo chenye ukubwa wa inchi 5.7 na ubora wa kioo ukiwa 1080 x 1920 pixels. Unapata kamera ya megapixels 8 upande wa mbele na kamera ya megapixel 13 nyuma. Fingerprint sensor imehamishiwa upande wa mbele juu ya “home button”.

Vifaa na Programu

Infinix Note 4 Pro inatumia Android 7.0 (Nougat) yenye prosesa ya Octa-core 1.3GHz inayoifanya simu hiyo kuwa nyepesi wakati wa kuperuzi mtandaoni au wakati wa kucheza gemu na kuifanya simu kutokuwa nzito pia ina RAM GB 3 na uwezo wa uhifadhi wa ndani wa 32GB. Unaweza kuweka memori kadi ya ziada mpaka GB 128.

SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Tecno Camon CX Air bei na Sifa zake

Ingawa Note4 ilipunguza nguvu ya betri kuwa 4300 mAh ukifananisha na Infinix Note 3, simu ya Infinix Note 4 Pro ina nguvu ile ile ya betri yani 4500 mAh.

Infinix Note 4 Pro ina Bluetooth 4.2, micro USB, dual-band Wi-Fi, na 4G LTE. Inategemea na eneo lako, kiwango cha LTE bands kinachopatikana kwajili yako kitatofautiana.

Bei na Upatikanaji

Infinix Note 4 Pro haijaanza kupatikana Tanzania , Kenya, ama Uganda. Ikianza kupatikana nchini Tanzania simu hii inategemewa kuuzwa kwa bei ya zaidi ya Tsh. 420,000.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako