Ifahamu Simu Mpya ya Vivo X21 Bei na Sifa Zake


Kampuni ya Vivo imekuwa na shughuli nyingi mwaka huu ikiwa tayari imezindua simu za mkononi aina mbalimbali. Unaikumbuka Vivo X20? Naam simu hii ni mrithi wake. Vivo X21 ilizinduliwa pamoja na Vivo X21 UD, aina nyingine ambayo tofauti yake ni sehemu ilipo fingerprint sensor tu. Simujanja mpya pia ina “notch” kama vile Vivo V9 iliyotolewa hivi karibuni, zote mbili zimeiga muundo wa iPhone X .

Uwezo na Sifa Muhimu za Vivo X21

  • Kioo: 6.28, Super AMOLED capacitive touchscreen, 2280 X 1080 pixels (402 ppi)
  • Processor: Octa-core Qualcomm SDM660 Snapdragon 660 CPU
  • RAM: 6GB
  • Memori: Hifadhi ya ndani ni 64GB/128GB, unaweza kuweka memori kadi hadi ya 256GB
  • Kamera: kamera ya nyuma ni Dual 12MP + 5MP  na kamera ya mbele ni 12MP
  • 4G LTE
  • Usalama: Fingerprint sensor (rear)
  • Betri: 3, 200mAh non removable Li-ion battery

Muonekano na Kioo

Vivo X21 ina muonekano wa kuvutia. Pia ni nyembamba na ina uzito wa karibu 156g na unene wa 7.4mm. Upande wa nyuma, kuna kamera zilizopangwa kuelekea chini na flash chini yake. Pia kuna fingerprint sensor iliyowekwa katikati kuelekea sehemu ya juu ya simujanja hii.

Kwa upande wa kioo inatumia skrini ya AMOLED, simujanja hii inakuja na kioo cha inchi 6.23 ( 2280 X 1080 pixels) na uwiano wa 19:9.

Betri na Kamera

Linapokuja swala la maisha ya betri, simujanja hii inakuja na betri yenye uwezo wa kawaida ukilinganisha na simu zingine ambazo ni “mid-range”. Vivo X21 inakuja na uwezo wa betri wa 3, 060mAh ambayo ina uwezo wa kuchaji kwa haraka kupitia USB Type-C port.

Utafurahia kupiga picha kwa kutumia simu hii kwani ina kamera mbili za nyuma, kitu ambacho kimeanza kuwa cha kawaida kwenye simu za bei ya chini. Nyuma ina kamera ya 12MP + 5MP na 12MP ya kamera ya mbele.

Vifaa na Programu

Simujanja hii inafanya kazi vizuri ikiwa na Qualcomm SDM660 Snapdragon 660 processor na Adreno 506 GPU kwajiri kucheza gemu na masuala mengine yanayohusiana na graphics.

Vivo X21 inakuja na RAM ya 6GB iliyounganishwa na hifadhi ya ndani ya 64GB au 128GB  inayoweza kupanuliwa hadi 256GB kwa kutumia memori kadi. Inatumia mfumo wa uendeshaji wa Funtouch OS 4.0 ambao upo kwenye Android 8.1 Oreo.

Bei na Upatikanaji

Vivo X21 inapatikana sasa nchini China lakini bado unaweza kununua yako kwenye maduka mbalimbali ya mtandaoni kwa karibu na Tsh 1,045,000 na Tsh 1,150,000 kwa 64GB na 128GB kwa mtiririko huo.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA