Ifahamu Simu Mpya ya Vivo V9 Bei na Sifa Zake


Ni jambo la kawaida kwa simu za mkononi zinazotumia mfumo wa Android kuiga muundo wa iPhone, simujanja nyingi sasa zinaiga muundo wa iPhone X. Simujanja kutoka kwa watengenezaji wa simu za mkononi kama Asus Zenfone 5 na Oppo F7 tayari zina kipengele kama hicho. Simu mpya ya Vivo V9 ni simujanja nyingine yenye “notch” na kwa hakika ina mwonekano mzuri. Ingawa ni tofauti na flagship ya Apple, simu janja hii ni “mid-range smartphone”. Hata hivyo, ina idadi nzuri ya vipengele ambavyo tutaviangalia kadri tunavyoendelea.

simu za vivo

Uwezo na Sifa Muhimu za Vivo V9

  • Kioo: 6.3-inch, IPS LCD capacitive touchscreen, 2280 X 1080 pixels (400 ppi)
  • Processor: Octa-core Qualcomm MSM8953 Snapdragon 626 CPU
  • RAM: 4GB RAM
  • Memori: Hifadhi ya ndani ni 64GB, unaweza kuweka memori kadi hadi ya 256GB
  • Kamera: kamera ya nyuma ni Dual 16MP + 5MP  na kamera ya mbele ni 24MP
  • 4G LTE
  • Usalama: Fingerprint sensor (rear)
  • Betri: 3, 260mAh non removable Li-ion battery

Muonekano na Kioo

Hakuna utata kwamba Vivo V9 ina muonekano mzuri hasa kwa kuwa na “notch” kwenye kioo ambayo ni ndogo kuliko ile ya iPhone X. Pia ina vitu vyote muhimu kama sensors, kamera na notification indicator. Simujanja hii imetengenezwa kwa plastiki.

Pia ina kioo cha inchi 6.3 (2280 X 1080 pixels). Kioo chake kina ukubwa nzuri na kunakupa uhuru zaidi wakati wa kucheza game au kuangalia filamu.

Betri na Kamera

Linapokuja swala la maisha ya betri, simujanja hii inakuja na betri yenye uwezo mzuri ukilinganisha na simu zingine ambazo ni “mid-range”. Vivo V9 inakuja na uwezo wa betri wa 3, 260mAh ambayo ina uwezo wa kuchaji kwa haraka.

Utafurahia kupiga picha kwa kutumia simu hii kwani ina kamera mbili za nyuma, kitu ambacho kimeanza kuwa cha kawaida kwenye simu za bei ya chini. Nyuma ina kamera ya 16MP + 5MP na 24MP ya kamera ya mbele.

Vifaa na Programu

Simujanja hii inaendelea kufanya kazi vizuri ikiwa na SoC ya uwezo wa kati ya Qualcomm. Inakuja na  Octa-core Qualcomm MSM8953 Snapdragon 626 CPU na Adreno 506 GPU kwajiri kucheza gemu na masuala mengine yanayohusiana na graphics.

Vivo V9 inakuja na RAM ya 4GB iliyounganishwa na hifadhi ya ndani ya 64GB inayoweza kupanuliwa hadi 256GB kwa kutumia memori kadi. Kwa kuongezea, simujanja hii inakuja na mfumo wa uendeshaji wa Android 8.1 Oreo na Funtouch OS 4.0 UI.

Bei na Upatikanaji

Vivo V9 inapatikana kwa manunuzi ya awali kwenye Duka la Vivo la mtandaoni na maduka mengine pia kwa bei karibu na Tsh 820,000 inategemea na eneo ulilopo.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA