Shirika la ndege la Ethiopian Airlines la nchini Ethiopia limetangaza safari yake ya kwanza ya ndege kwenda nchini Nigeria ambayo itaongozwa na wanawake pekee kuanzia marubani, wahudumu, mafundi mitambo pamoja na waongoza ndege.

Ndege hiyo itafanya safari hiyo leo December 16, 2017 kutoka Addis Ababa Nigeria hadi Lagos Nigeria ikiwa na baadhi waandishi wa habari ili kuripoti jinsi safari nzima ilivyokuwa.

Inaelezwa kuwa hii itakuwa ndege ya kwanza kuongozwa na wanawake pekee barani Afrika.

Moja ya marubani Capt. Amsale Gualu amenukuliwa akisema “Hii ndege itaonesha wanawake juwa kama tutapata fursa na kufanya kazi kwa bidii, tunaweza kufanikiwa kwenye jambo lolote na katika eneo lolote la taaluma hata kwenye tasnia ya anga.”

Sambaza:

Written by Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako