Intaneti

Ifahamu Facebook ya bure kutoka Vodacom Tanzania

on

Mitandao mingi ya simu hivi sasa inatoa huduma ya facebook ya bure, lengo ni kuendeleza nia ya kutoa huduma bora na nafuu kwa wateja.

Facebook ya bure

Leo nitatoa ufafanuzi kuhusu kuhusu vigezo na Masharti ya Free Facebook kutoka vodacom:

Facebook bure ni nini?

Facebook bure inawawezesha wateja wote wa Vodacom kutumia Facebook Flex bure kabisa bila makato yoyote. Utaweza kuchati, ku-comment, ku-like na ku-share matukio bure. Wateja wa malipo ya awali wanaonunua vifurushi vya intaneti pia watapata picha bure kwenye Facebook mpaka bando (kifurushi) kitakapokwisha.

Nani anaweza kufurahia Facebook bure?

Mteja yoyote wa Vodacom wa prepaid, hybrid, au postpaid anaweza kufurahia ofa hii kabambe. Cha kufanya, tembelea www.facebook.com au tumia App ya Facebook kwenye simu yako ya Android ufurahie Facebook bure! Ni rahisi kabisa. Wateja wanaonunua vifurushi vya intaneti vya Vodacom pia watapata picha bure kwenye Facebook mpaka kifurushi kitakapokwisha.

SOMA NA HII:  Opera CEO: Kuiuza Opera kwa Kampuni za China Haikuwa Uamuzi Wetu

Unatumia vipi facebook ya bure?

Kutumia Facebook bure na Vodacom, mteja utatakiwa kuingia kwenye akaunti yako ya Facebook kupitia www.facebook.com kwenye browser [kivinjari chochote] yoyote au kwa kutumia App ya Facebook kwenye simu yako ya Android.

Ikiwa huna Facebook unaweza kutengeneza akaunti ya Facebook kupitia www.facebook.com, kisha jaza jina lako, jaza namba ya simu au barua pepe kisha tengeneza namba ya siri. Ndani ya zisizozidi dakika 5 utaweza kuenjoy Facebook bure na kuunganisha na uwapendao na ku-share matukio muhimu bure kabisa!

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published.