Ripoti : Idadi ya watumiaji wa Intaneti yaongezeka Kufikia milioni 23


Ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ya mpaka Desemba 2017 imeonesha kuwa idadi ya watumiaji wa intaneti imeongezeka kufikia watu milioni 23 ambayo ni sawa na asilimia 45 ya Watanzania wote.

Takwimu imeonesha kuna ongezeko kubwa la watumiaji wa Intaneti mwaka hadi mwaka. Takwimu ya mwaka 2012 ya watumiaji wa Intaneti ilikuwa ni milioni 7.52 ambayo ni asilimia 17 wakati mwaka 2013 wakaongezeka kufikia milioni 9.31 sawa na asilimia 21.

[irp]

Mwaka 2014 watumiaji walifikia milioni 12.17 sawa na asilimia 29, mwaka 2015 watumiaji waliongezeka kufikia milioni 17.62 sawa na asilimia 34 na mwaka 2016 idadi ilifika milioni 19.86 sawa na asilimia 40.

Ripoti hiyo pia inaonesha kuwa idadi ya watumiaji wa simu za mkononi imefikia milioni 40 kutoka milioni 27.62 mwaka 2012, huku mtandao wa Vodacom ukiongoza kwa kuwa na watumiaji waliojisajili 12,714,297 wakifuatiwa na Tigo kwa kuwa na watumiaji waliosajiliwa 11,062,852.

[irp]

Katika aina ya intaneti inayotumika, watu 19,006,223 wanatumia intaneti ya ‘wireless’ inayohamishika kama simu, 3,468,188 wanatumia intaneti ya ‘wireless’ isiyohamishika na wale wa wanaotumia wired idadi yao ni  520,698.

Je una mtazamo gani juu ya idadi hii? Je ongezeko la watumiaji linatokana na watu wengi watumiaji wa intaneti kuwa na simu mbili au ata zaidi ?

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA