Nyingine

Huyu ndio mwanafunzi wa Iran anayefananishwa na Lionel Messi

Reza Parastesh ni mwanafunzi kutoka nchini Iran anayefananishwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina anayeichezea FC Barcelona ya Hispania Lionel Messi.

Reza Parastesh, mwenye umri wa miaka ishirini na tano kwa sasa, hivi karibuni ameanzisha mtindo wa ukataji nywele na kupunguza ndevu zake kama mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Argentina . Hali inayopelekea watu wa mji wa Hamaden-Iran kumfananisha na nguli huyo ya mpira wa miguu.

Kijana huyo alianza kufananishwa na Messi miezi michache iliopita, watu kumzonga wengine wakihisi ni Lionel Messi kutokana na jezi na style ya nywele na ndevu zake kuziweka kama Messi, Reza Parastesh alichukuliwa na Polisi na kufikishwa kituoni kutokana na kusababisha usumbufu na msongamano.

Kijana huyo amesema:

Kwa sasa watu wananiona kama Lionel Messi na wanataka nifanye vitu kama anavyofanya yeye na ninapofanya baadhi ya vitu watu wanashtuka sana, nina furaha sana wakiniona mimi wanafurahi furaha ambayo mimi inanipa nguvu” >>>> Reza Parastesh

Soma na hizi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close