Sambaza:

Ukweli ni kuwa, kuna wakati ambao tunahitaji kufuta picha kwenye Instagram pengine kwa sababu tunahisi picha haionekani vizuri tena. Hata hivyo, kufuta picha pia ina maanisha kufuta “likes na comments”  kwenye picha hiyo, inasikitisha kwa sababu unaelewa muda na nguvu uliyotumia kupata vitu hivyo.

Sasa, inabidi tuishukuru Instagram, kwa sababu haihitaji tena kuzifuta kwa sababu wameanzisha kipengele kidogo kinachokuwezesha kuficha picha zako za zamani katika mtazamo wa umma na kukupa uwezo wa kuzirudisha kwa urahisi siku zijazo kama utapenda.

Ili kutumia kipengele hiki, Kwanza update Instagram programu yako na kisha kuchagua picha unayotaka kufanya kutoweka. Chaguo la archive huonekana chini ya “three dotted menu.”

Tofauti na kufuta picha, picha hizi utakazoziweka kwenye kumbukumbu zitaendelea kuwepo kwenye  folda lako la faragha ( huku “likes na comments” zikiendelea kuwepo), hili folda lako binafsi lina alama ya “Rewind Clock” icon.

Unaweza kuchagua kurejesha picha, kufuta kabisa, au kushiriki wenzako kwenye Whatsapp.

Kama nilivyosema, kipengele kidogo ila kina umuhimu sana.

Kuna mtu yeyote tayari amejaribu huduma hii?


Sambaza:
SOMA NA HII:  Orodha ya njia za mkato za keyboard katika Mozilla Firefox

This article has 2 comments

  1. Amani Reply

    Shukrani sana kaka kwa kutujuza, Ila bado sijajaribu ila nitafanya hivyo kwani nimeshafanya “update” kwenda kwenye toleo jipya. Naona Instagram wanaleta huduma nzuri kwa watumiaji wake.

    • salim Reply

      Mkuu mimi nimejaribu inafanya kazi naona instagram wanazidi kujiimarisha

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako