Tanzania Telecommunications Company Ltd (TTCL) imeweka malengo yake kuwa na uwezo wa kutoa huduma za 4G LTE nchini nzima ifikapo mwaka 2018, kampuni ya TTCL inajaribu kufufua ngome yake kwa kutoa huduma bora na za kisasa. Shirika – sasa lipo chini ya udhibiti kamili wa serikali – tayari imezindua huduma za 4G jijini Dar es Salaam na sasa inatarajia kuharakisha upatikanaji wake.

ttcl 4g

Msemaji wa kampuni Nicodemus Mushi, ameliambia gazeti la Citizen kuwa hivi karibuni itaunganisha taasisi za umma, mashirika ya kiraia “civil society organisations (CSOs)” na watumiaji binafsi na mtandao wa 4G-LTE wa haraka sana ili kurahisisha mawasiliano yao ‘.

SOMA NA HII:  Airtel Money yatangaza gawio la bilioni 1.7 kwa wateja

Mr Mushi alionyesha idadi ya mikoa ambayo itafaidika na mpango huo katika awamu ya kwanza, yaani: Arusha, Iringa, Mbeya, Dodoma, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Tanga, Kilimanjaro na Unguja. ‘Kwa kupitia mpango mkakati wetu wa biashara¬† tunatarajia kuongeza uwepo wetu katika soko kwa kuhakikisha kwamba tunatoa huduma zilizobora na kuongeza uwajibikaji na ufanisi,’ alisema.

TTCL ilizindua mtandao wake wa data ya simu ya 4G LTE (4G LTE mobile data network) mnamo Disemba 2015 na mpango wa miaka mitano wa kufikia mikoa yote na barabara kuu nchini. Mwezi uliopita ilitangaza kuwa inaongeza “LTE cell sites” 50 jijini Dar es Salaam ili kuboresha kasi ya data na upatikanaji wake. Maboresho hayo yatafanya kuwe na idadi kamili ya maeneo yenye LTE hadi 75.

SOMA NA HII:  Ifahamu Timu ya Mwitikio wa Kukabili Majanga ya Kompyuta Tanzania TZ-CERT

Mkuu wa Biashara wa Kampuni, Jane Mwakalebela, alisema wakati huo: “Tulianza kwa kuanzisha maeneo kumi na moja katika jiji, kisha tuliongeza maeneo mengine 14 , lakini mahitaji ni makubwa sana. Tunaanza kuzindua huduma sawa na maeneo ya ziada ya 50 katika jiji. “Baada ya kupanua, TTCL tunapanga kuanzisha teknolojia ya 4G kwa mikoani, Mwakalebela pia alisema kuwa kampuni inafanya maandalizi yake ya mwisho kabla ya kuanzisha¬† huduma za sauti LTE.

Sambaza:

Written by Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako