Mawasiliano

Huduma ya kuhama mtandao bila ya kubadili namba yaanzishwa Tanzania

on

Huduma ya Mobile Number Portability itaanza rasmi Tar 01 March 2017. Huduma hii itakuwezehsa kuhamia mtandao wowote ule bila kubadilisha namba yako:

mtandao-mediahuru

Kutokana na umuhimu wa tekinolojia ya habari na mawasiliano (Tehama) katika maendeleo ya taifa, mijini na vijiji TCRA imezindua mpango maalumu wa kuhama mtandao mmoja wa simu kwenda mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu na kueleza njia za kufuata ili kupata huduma hiyo.

Huduma hiyo inampa fursa mteja kuhama kutoka mtandao mmoja wa simu kwenda mwingine bila kubadili namba na uhamaji huo unatakiwa kuwa wa hiari na si kulazimishwa au kuzuiliwa kuhama.

SOMA NA HII:  TCRA imezindua mfumo wa usajili laini kwa kutumia alama za vidole

Huduma hiyo pia itaongeza ushindani kwenye sekta ya mawasiliano na hivyo kuwa kichocheo cha utoaji huduma bora. .

NB:Huu ndo muda wa makampuni ya simu kuboresha huduma zao. Watu wengi walishindwa kuhama mtandao kwa kuhofia namba zao.

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published.