Huawei P20 Lite vs P10 Lite – Bei na Sifa


Simu ya Huawei P20 Lite haikupewa kipaumbele na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi wake wa kimataifa, lakini ina uwezo wa kuwa moja ya simu zitakazofanya vizuri katika soko la Tanzania.

Mtangulizi wake, P10 Lite, ilikuwa moja ya simu za Huawei zilizofanya vizuri zaidi kwa mwaka jana, kwa sababu ya bei yake na sifa za kuvutia.

Huawei P20 Lite ina mwonekano wa kisasa unaofanana na simu ya P20 na P20 Pro na pia ina vipengele vipya.

Vifaa

Simu mpya inakuja na vifaa vya kuvutia ikilinganishwa na mtangulizi wake, ikiwa ni pamoja na “bezel-less display” na kamera ya nyuma ya lensi mbili.

P20 Lite inajumuisha 64GB ya hifadhi ya ndani na 4GB ya RAM, Sifa na bei ya Huawei P10 Lite na P20 Lite zimewekwa hapa chini.

SIFA Huawei P10 Lite Huawei P20 Lite
Vipimo 146.5 x 72 x 7.2 mm 148.6 x 71.2 x 7.4 mm
Uzito 146g 145g
Mfumo wa Uendeshaji (OS) Android 7.0 Android 8.0
Kioo 5.2-inch 1,080 x 1,920 IPS LCD 5.84-inch 1,080 x 2,280 IPS LCD
Kamera ya Nyuma 12MP Dual 16MP + 2MP
Kamera ya Mbele 8MP 16MP
Hifadhi 32GB, microSD 256GB 64GB, microSD 256GB
RAM 3GB 4GB
Processor 2.1GHz + 1.7GHz Octa-core Kirin 658 2.36GHz + 1.7GHz Octa-core Kirin 659
Betri 3,000mAh 3,000mAh
Mtandao LTE LTE
SIM Nano (Single/Dual) Nano (Single/Dual)
Biometrics/Ulinzi Fingerprint Fingerprint, facial recognition
Bei (inategemea na eneo ulilopo)
Tsh 950,000 Tsh 1140,000

Vipengele vipya

Simu ya P20 Lite sio tu ina vifaa bora kuliko P10 Lite, bali inajumuisha uwezo ulioboreshwa zaidi na vipengele vipya vya programu.

Mashabiki wa Android Oreo watafurahi kusikia kwamba simu hii inakuja na Android 8.0 moja kwa moja, na ina uwezo wa “picture-in-picture viewing” na sifa zingine za kuvutia.

Simu hii pia ina mfumo wa kiusalama wa kutambua sura unaotumiwa kwa kamera yake ya mbele ya 16MP, mfumo huu unakuwezesha kufungua simujanja yako kwa kuiangalia tu.

Huawei P20 Lite pia ina uwezo wa kuchaji kwa haraka na sasa kupitia USB-C badala ya micro-USB.

Ina uwezo wa kuunganisha vifaa viwili kwa wakati mmoja kupitia Bluetooth, ingawa bei yake ipo juu zaidi kuliko bei ya P10 Lite, P20 Lite ina mwonekano wa kipekee na  vipengele vilivyoboreshwa zaidi.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA