Simu za Mkononi

HTC yazindua simu mbili mpya HTC U11+ na U11 Life

on

Rafiki mpya wa Google ameongeza simu mbili mpya – HTC U11 +:

Na U11 Life:

U11+ ina ukubwa tofauti na toleo la zamani la U11 na ina vitufe vidogo, wakati U11 Life iko kwenye jamii ya kati na inakuja katika matoleo mawili – Android One na Sense.

Kwa upande wa vipengele na sifa zingine, HTC U11 + ni kifaa chenye kioo chenye ukubwa wa inchi 6 na Quad HD (2,560 x 1440 pixels) Super LCD inawezeshwa na prosesa aina ya Snapdragon 835 2.45GHz octa-core chip, uwezo wa RAM na ROM ni RAM 4GB / 64GB ROM au 6GB RAM / 128GB ROM na betri 3,930mAh. Kamera ya nyuma kwenye HTC U11+ ina megapixel 12 na kamera ya mbele ni megapixel  8.

SOMA NA HII:  Unamiliki simu ya iPhone ? Apple inapunguza kasi ya simu yako

Kwa upande wa HTC U11 life ni kama binamu wa HTC U11. Kutokana na sifa zake. Sifa kamili za HTC U11 life ni kama ifuatavyo:

 • Prosesa: Qualcomm Snapdragon 630 octa-core
 • Kioo: 5.2 inchi 1080×1920 pixels resolution Super LCD na Gorilla Glass
 • Mfumo Endeshi (Operating system): Android 7.1.1 Nougat ikiwa na HTC Sense
 • RAM: 3GB
 • Ujazo wa ndani (Storage): 32GB pia unaweza kuweka memori
 • Uwezo wa Kuzuia maji na vumbi: IP67
 • Kamera: Kamera ya nyuma (Rear) 16 megapixel, f/2.0 aperture camera. Kamera ya mbele (Selfie) 16-megapixel na f/2.0 aperture
 • Betri: 2600 mAh
 • Wireless connectivity: 802.11 a/b/g/n/ac WiFi, Bluetooth 5.0, NFC
 • Sensors: Fingerprint, G-Sensor, Gyroscope, Compass, Ambient Light, Proximity, Edge Sensor
 • Vipimo: 149.09 x 72.9 x 8.1 mm na uzito wa 142 gram

Sijui kuhusu wewe, lakini HTC U11 life imenivutia sana, kutokana na sifa za kamera yake ya kuvutia na bei nafuu, lakini sijapendezewa na HTC U11 +.

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published.