Simu za Mkononi

HTC U11 Life: Toleo jipya la simu janja kutoka HTC! #Uchambuzi

HTC U11 Life ni toleo dogo la U11 kwajili ya wanunuzi ambao wanataka kitu cha bei nafuu zaidi. Inakuja na processor isiyo na nguvu sana lakini bado ni imara na ina teknolojia inayofanana ya Edge Sense.

Uwezo na Sifa za HTC U11 Life

  • Prosesa: Qualcomm Snapdragon 630 octa-core
  • Kioo: 5.2-inch Super LCD Display, 1080 x 1920 pixels (424ppi)
  • Mfumo Endeshi (Operating system): Android 8.0 (Oreo), HTC Sense UI
  • RAM: 3GB/4GB
  • Ujazo wa ndani (Storage): 32GB/64GB pia unaweza kuweka memori hadi 256GB
  • Kamera: Kamera ya nyuma (Rear) 16 megapixel,Kamera ya mbele (Selfie) 16-megapixel
  • Betri: 2600 mAh
  • 4G LTE (hadi 600Mbps)
  • Wireless connectivity: 802.11 a/b/g/n/ac WiFi, Bluetooth 5.0, NFC
  • Sensors: Fingerprint, G-Sensor, Gyroscope, Compass, Ambient Light, Proximity, Edge Sensor
SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Infinix S2 Pro X522 bei na Sifa zake

Muundo na skrini

Hii ni chaguo bora kuliko HTC U11 linapokuja swala la kuitumia na mkono mmoja. Vipimo vya smartphone ni 149.1 x 72.9 x 8.1 millimita. Itakuvutia zaidi kwenye upande wa fingerprints. Ina kiwango cha IP67, maana yake ni kwamba inazuia vumbi na maji.

Kwa mbele, HTC U11 Life ina kioo cha HD chenye inchi 5.2 kwa juu kina Corning Gorilla Glass

Kamera

Smartphone hii ya uwezo wa kati ina kamera zenye 16MP – moja mbele na nyingine nyuma. Kamera zote mbili zina ukubwa wa f / 2.0. Vipengele vya kamera ni pamoja na autofocus, LED flash na HDR. Shooter kuu inarekodi video za ubora wa 4K. Unaweza pia kupiga video za HD (1080p) na snapper ya selfie mbele ya HTC U11 Life.

Utendaji na OS

Kwa upande wa processor, HTC U11 Life haitumii Qualcomm Snapdragon 835 kama U11. Inatumia octa-core Snapdragon 630 chipset ambayo inaendesha kwa kasi hadi 2.2 GHz. Lakini kwa GB 3 au 4 GB ya RAM simu hii bado ina uwezo wa kufanya kazi vizuri.

Kuna GB 32 au 64 GB ya uhifadhi ndani ya simu, inategemea na toleo utakalo nunua. Uhifadhi pia unaweza kuongezwa kwa kuweka memori kadi . HTC U11 Life inatumia mfumo wa hivi karibuni wa Android 8.0 Oreo.

Sifa nyingine na Uwezo

Teknolojia ya ubunifu ya Edge Sense ya HTC inapatikana pia kwenye hii simu. Inakuwezesha kufanya kazi mbalimbali kwa wakati mmoja. Unaweza kutumia kuchukua selfies, kufungua Google Assistant au kufanya kazi nyingine.

HTC U11 Life ina safu ya kushangaza ya vipengele vya kuunganishwa, ikiwa ni pamoja na 4G LTE. Betri yake sio nzuri sana kwani ina uwezo wa 2,600 mAh.

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako