Sambaza:

Unatafuta simu ya mkononi ambayo itakuwa nzuri kwako kama mpenzi wa muziki ? Mediahuru tumekusogezea orodha ya simu janja (smartphones) bora kwa wapenzi wa muziki.

HTC 10

Simu hii ina 24-bit DAC (Digital-to-Analog Converter), imeunganishwa na headset amp ndani yake, ambayo inakupa uzoefu wa kusikiliza muziki wenye ubora kama miaka ya nyuma ‘siku za kupenda sauti ya analog’.

Ina spika zenye nguvu na inatumia mfumo wa Hi-Res, ina uzito wa 161g, vipimo vya 145.9 x 71.9 x 9 mm, ukubwa wa skrini wa inchi 5.2, 4GB RAM, 32GB ya uhifadhi na kamera ya mbele ya 5MP na ya nyuma ya 12MP. Pia, kila spika yake ya BoomSound Hi-Fi ina amp zake na mipangilio binafsi ya tweeter na ya woofer.

SOMA NA HII:  Nafasi za ajira serikalini sasa kuwafikia wahitimu kwa simu ya mkononi

Sony Xperia XZ Premium

Sisi sote tunajua kuhusu urithi wa Sony ‘Walkman’, kwa hiyo sio ajabu kwamba Sony ni ‘moto wa kuotea mbali kwenye ubora wa sauti ya simu’. Sony Xperia XZ Premium ina app ya muziki ambayo ni mojawapo ya music players  bora inayopatikana kwa sasa, na inawezeshwa na Hi-Res audio.

Sifa zake za msingi ni pamoja na: uzito (195g), dimensions (145.9 x 71.9 x 9 mm), ukubwa wa skrini (5.5-inch), RAM (4GB), kuhifadhi (64GB), kamera ya nyuma (19MP) na kamera ya mbele (13MP). Kitu kikubwa kuhusu Xperia XZ Premium ni Digital Sound Enhancement Engine (DSEE HX), ambayo ina uwezo wa ku-upscale nyimbo zilizopo kufikia ubora wa Hi-Res. Zaidi ya hayo, unaweza pia kuhamisha Hi-Res audio kupitia Bluetooth.

SOMA NA HII:  Simu bora za Infinix na Bei zake nchini Tanzania

Samsung Galaxy S8

Hii ni moja ya simu bora zaidi ulimwenguni ili kuonekana kwake kwenye orodha hii inaweza kuwa si jambo la kushangaza. Sifa zake za msingi ni pamoja na: uzito (155g), vipimo (148.9 x 68.1 x 8mm), ukubwa wa skrini (5.8-inch), RAM (4GB), uhifadhi (64GB), kamera ya nyuma (12MP) na kamera ya mbele (8MP).

Samsung Galaxy S8 inajumuisha uunganisho wa Bluetooth 5 na moja ya vipengele vyake muhimu kuwa Bluetooth Dual Audio, ambayo inakuwezesha kuunganisha jozi mbili za wireless Bluetooth headphones kwenye simu moja wakati huo huo. S8 pia ina uwezo wa Hi-Res audio, ambao unakuwezesha kufurahia sauti yenye ubora wakati wote.

SOMA NA HII:  Njia rahisi kabisa ya kuroot simu yako ya Android

LG V20

Hii inajulikana zaidi kama ‘audio powerhouse’. Ina mpangilio wa quad-DAC unaowezeshwa na ESS Sabre ES9218 chip, mfumo unaopeleka uzoefu wako wa kusikiliza muziki kwenye kiwango bora zaidi

Sifa zake za  msingi ni pamoja na: uzito (174g), vipimo (148.9 x 68.1 x 8mm), ukubwa wa skrini (5.7-inch), RAM (4GB), uhifadhi (32 / 64GB), kamera ya nyuma (16MP na 8MP) na kamera ya mbele ( 5MP).

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako