Nyingine

Hii orodha mpya ya viwango vya soka duniani FIFA, Tanzania yashika nafasi ya 135

Shirikisho la Soka Duniani, (FIFA) limetoa orodha ya viwango vya soka kwa wanaume duniani vya mwezi huu, ambapo kwa mujibu wa orodha hiyo, Tanzania imeendelea kushikilia nafasi ya 135 kama ilivyokuwa mwezi uliopita.

FIFA

Mwezi uliopita Tanzania Ilipanda kwa nafasi 26 kufuatia kushinda mechi mbili mfululizo dhidi ya Botswana na Burundi.

Kwa ukanda wa Afrika Mashariki, Uganda wameendelea kuongoza kwa kukamata nafasi ya 72, wakifuatiwa na Kenya ( 78 ) kwenye viwango vya Dunia.

Brazil bado ni vinara kwa nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Argentina nafasi ya pili,nafasi ya tatu ni Ujerumani,nafasi ya Nne ni Chile, nafasi ya tano ni Colombia ,nafasi ya sita ni Ufaransa,nafasi ya saba ni Ubeligiji, nafasi ya nane ni Ureno ,nafasi ya tisa ni Switzerland na nafasi ya kumi ni Hispania.

Kwa upande wa Afrika Misri bado ni vinara ikiwa katika nafasi ya 19 Ulimwenguni, na orodha nyingine ya ubora Duniani itatoka tena Juni Mosi.

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also

Close