Uchambuzi

Hii ndio simu mpya ya Tecno Phantom 8. Sifa na Bei yake kwa Tanzania

Tecno Phantom 8 ni mrithi wa Phantom 6 na 6 Plus ambazo ziliachiliwa hapo septemba 2016. Wakati huu, kampuni hiyo haikuacha tu kutoa toleo namba 7, lakini imetoa toleo moja la simu, bila chaguo la Plus. Kuna maboresho mapya ndani ya simu hii, moja kati yao ni kamera mbili za nyuma na uwezo wa telephoto pamoja na RAM kubwa ya 6GB. Angalia vipengele vyote hapa chini.

Boksi la Phantom 8 lina nailoni hivi imelizunguka boksi ili kulilinda na vumbi pamoja na unyevunyevu.​ Boksi lake ni jeusi na sio kubwa kivile kama la Phantom 6 plus. Lina nembo ya Phantom 8 kila upande.

Baada ya kufungua boksi, unakutana na simu ya Phantom 8 ikiwa imetulia vizuri katikati ya viboksi viwili vyenye vifaa vingine vinavyokuja na Phantom 8.

Hakika simu hii imejitosheleza. Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo vimeambatana ndani ya boksi:

 • Simu yenyewe ya Phantom 8
 • Kichwa cha chaji na waya wa USB Type C
 • Earphones
 • Kijitabu cha jinsi ya kutumia simu
 • Kava la simu (Sio la kufunga na kufungua, transparent)
 • Kipini cha kutolea line

Pia kuna zile documents hivi kama warranty card, kadi ya Boom play. Tecno pia wametuwekea kava la nyuma buree kabisa pamoja na screen protector.

Ina Fast charger kabambe kabisa na waya wa USB Type C na Earphones maridhawa kabisa. Tuachane na hizo accessories sasa, twende kukiangalia kifaa chenyewe kwa uzuri kabisa. Binafsi kitu cha kwanza ambacho kimenikosha ni hii mambo wenyewe wanaita 4GLTE worldwide roaming. ​Hii inamaanisha waweza tumia Phantom 8 popote pale duniani.

SOMA NA HII:  Mambo Muhimu Yanayo Tarajiwa Kuja Kwenye Simu Mpya Ya Samsung Galaxy S9

​Kuna haka protector transparent ya nailoni kwa mbele na nyuma ya kuzuia simu isipate scratch.

​Kifaa chenyewe ni chepesi na kinashikika vizuri kabisa kutokana na 5.7 inch display iliyonayo. Juu ya kioo kuna kamera ya kutwanga maselfi yenye 20 MP, spika kwa ajili ya calls na dual flash lights.

Kwa nyuma sasa wamesimama malegendari wenyewe kamera mbili 13 MP & 12 MP Refocusing camera pamoja na tri Flash na fingerprint scanner.

​Kwa upande wa kulia wa simu kuna button ya power na zile za sauti.

Sehemu ya kuwekea line ipo upande wa kushoto na unaweza kuitoa kwa kutumia kile kipini ambacho kimekuja na boksi tayari.

​Unaweza ukatumia line mbili zote kwa pamoja, au line moja na memory card. Huwezi kuweka line mbili na memory card kwa wakati mmoja.

Kuna katundu cha kuchomeka earphone kwa juu kama ilivyo kwenye simu zingine za Tecno.

Spika, mistari ya antenna, mic na port ya kuchajia vyipo kwa chini.


Kuiwasha kwa mara ya kwanza pamoja na kuiseti ni rahisi sana. Phantom 8 imekuja na Android 7.0 Nougat pamoja na HIOS 3.0.

Kwa ujumla Phantom 8 ni kifaa cha ukweli kabisa kulingana na nilivyokiona na kukitumia kidogo kwa mara ya kwanza, ni dhahiri kabisa kua Tecno wamefanya kazi nzuri.

SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Tecno W3 bei na Sifa zake

Sifa za Phantom 8

  Tecno Phantom 8
Display 5.7 inchIPS LCD

1080*1920

Full HD

Internet 3G, 4G LTE
Camera Rear: Dual 12MP+ 13MP (one is a telephoto lens)Tri- LED Flash

Front: 20MP with Dual-LED flash

OS Android 7.0 Nougat , HiOS 3.0
CPU Octa core 2.6 GHz, A53Mediatek Helio P25 (16nm)
GPU Mali 880 MP2
RAM 6GB RAM
Storage 64GB
Battery 3500mAh with fast charge
Body 159.9*79.5*7.9mmDiamond Fire design
Colours Phantom Black, Galaxy Blue, Champagne Gold
Special features · Dual rear camera with 2X optical zoom and 10X digital super zoom· 6 GB RAM for fluid multitasking

· Diamond Fire design that has a shiny back that reflects light beautifully

· Fast charge; 0-100% in 70 minutes

· The 16nm Mediatek Helio P25 guarantees great battery life

· Global 4G LTE with speeds of up to 300mbps.

· Rear mounted fingerprint reader

· 3.5mm jack present

PRICE $400 (Tsh 866000)

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

8 thoughts on “Hii ndio simu mpya ya Tecno Phantom 8. Sifa na Bei yake kwa Tanzania”

  1. mkuu Ino Dama nafikiri mediahuru hawajaweka bei kwa sababu bado bei rasmi kwa Tanzania haijatangazwa kwa nigeria inauzwa ₦ 140,999 , kwa kenya ni KSh 36,999 nafikiri bei rasmi kwa bongo haitazidi 850000/=.

   1. Zipo mikoan zinauzwa laki tatu vip ni zenyewe kweli Hizo?
    Kuna jamaa katuma mtandaon na namba yake ninayo lakin naogopa kununua

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako