Nyingine

Hawa ni wachezaji 6 ambao watachukua nafasi baada ya Messi na Ronaldo kama wachezaji bora duniani

Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wameongoza tuzo za FIFA Ballon D’or awards kwa miaka nane iliyopita na sio rahisi mchezaji mwingine kuchukua nafasi yao kwa siku za karibuni.

Messi ana miaka 29 akizidiwa miaka miwili na  Ronaldo mwenye umri wa miaka 31. Wengi wanatabiri ya kuwa miaka mnne ijayo tutashuhudia mchezaji mwingine anashinda tuzo hii mbele ya wachezaji hawa.

Katika makala hii tunaangalia wachezaji wenye miaka 25 ama chini ya hapo, samahani Gareth Bale, haupo kwenye list hii.

Hawa ni wachezaji sita ambao wanaweza kumaliza utawala wa Ronaldo na Messi.

1. Neymar

Alikuwa wa tatu katika tuzo za FIFA Ballon D’or mwaka 2015  na anaendelea kuonyesha makali yake. Inatarajiwa kuwa atakuwa wa tatu tena mwaka huu baada ya kuiongoza Brazil kuchukua dhahabu katika Rio Olympics.

2. Eden Hazard

Uwezo wake ulishuka katika msimu 2015/2016 baada ya kuiongoza Chelsea kutwaa taji la Ligi Kuu  msimu wa awali lakini akiwa na miaka 25 amekuwa akionyesha makali yake na kujenga upya muda aliopotea wengi wanaamini amerudi kwenye ubora wake msimu huu.

Wengi walidhani angeweza kuwa mtu pekee wa kuwanyamazisha Messi na Ronaldo mpaka fomu yake iliposhuka.

3. Renato Sanches

Mshindi wa Golden Boy award mwaka 2016. Sanches anaweza kuchukua muda kukaa sawa ndani ya Bayern ila tayari ameonyesha ubora wake na huwezi kumpuuzia.

SOMA NA HII:  Marufuku Matumizi ya Takwimu za Kampuni ya Geopoll - Dkt. Mwakyembe

Akiwa na miaka 19 anatarajiwa kuwa mchezaji  bora zaidi katika soka miaka kumi ijayo.

4. Paul Pogba

Sahau kiwango chake msimu huu pale Manchester United na utaona uwezo mkubwa alionao Paul Pogba. Kuna sababu ya kwanini United waliamua kuweka record ya dunia kwa ajili  ya kumnunua mchezaji huyu kutoka nchini ufaransa.

Kama Mourinho ataweza kumtumia vizuri na kuonyesha uwezo wake, anaweza kushinda Ballon D’or bila ya wasiwasi.

5. Paulo Dybala

 

Tayari ameonekana katika timu ya taifa ya Argentina kama mrithi wa Lionel Messi. Alifunga mabao 19 katika mechi 34 katika klabu ya Juventus msimu uliopita na amefanikiwa kuubeba uwezo wake katika msimu mpya.

Jicho lake la kutoa pass na uwezo wake wa kufanya dribbling ni baadhi ya vitu alivyobarikiwa.

6. Antoine Griezmann

Alitangazwa kama mchezaji bora kwenye Euro 2016 mbele ya Cristiano Ronaldo na mchezaji bora wa La Liga mbele ya Messi na Ronaldo. Amewapita watu hawa kwenye La Liga na Ronaldo kwenye bara la ulaya , kinachofata ni kuiteka dunia.

* Maalum: Ousmame Dembele wa Dortmund (ana miaka 19-Mfaransa)
Unafikiri nani kati yao atachukua Ballon D’or na mchezaji bora wa dunia- FIFA ufalme wa Messi na Ronaldo utakapo kwisha?

Toa maoni yako.

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.