Hatua za Usalama Wakati Wa Kufanya Ununuzi Mtandaoni “Online”


Jinsi ya kuwa salama wakati wa kufanya ununuzi mtandaoni: Masoko ya mtandaoni yanazidi kuwa maarufu, tofauti na ilivyokuwa mwanzo. Watu wengi zaidi wanazidi kupendelea kufanya ununuzi kwenye majukwaa ya mtandaoni kama Amazon, Jumia, na Kupatana kwa sababu ya utofauti na urahisi wa kufanya ununuzi wa mtandaoni.

Kikwazo kwenye ununuzi wa mtandaoni ni udanganyifu wa Intaneti. Kuna hatari kubwa ya wadanganyifu kujiingiza kwenye majukwaa yenye usalama mdogo kwa lengo la kupata maelezo yako ya kibinafsi na kuyatumia kusababisha madhara kwako.

Hivyo ni muhimu kwa watu wote kujifunza na  kujua hatua za msingi za usalama ambazo zinaweza kuleta tofauti kati ya mnunuzi mwenye furaha mtandaoni na muathirika wa akaunti ya benki iliyovamiwa.

Ziamini “Secured Websites”

Kwa ujumla, tovuti ambazo zimechukua hatua ya kutumia HTTPS ni salama zaidi kuliko zile zinazotumia HTTP. HTTP ni kifupi cha Hypertext Transfer Protocol; mfumo wa kusafirisha data kwenye mtandao.

Hifadhi ya uhamisho wa data ya HTTP inalenga jinsi taarifa inavyowasilishwa, badala ya jinsi inavyoipata kutoka kwa mtumaji hadi kwa mpokeaji.

Kwa upande mwingine, HTTPS (Secure Hypertext Transfer Protocol) ilitengenezwa ili kuruhusu ubadilishanaji salama wa taarifa za siri. HTTPS inaongeza safu ya ziada ya usalama kupitia itifaki ya SSL (Secure Sockets Layer).

SOMA NA HII:  Safaricom kuruhusu kutuma na kupokea pesa kupitia PayPal

Lipa kwa Credit, sio Debit cards

Debit cards ni rahisi kuzitumia kufanya manunuzi kwa sababu unaweza kupunguza kikomo kwa ajili ya matumizi yako. Hata hivyo, zina usalama mdogo zaidi kuliko credit cards na zinaweza kudukuliwa kwa urahisi zaidi.

Epuka Ununuzi kwenye Mitandao ya Umma (Public Networks)

Kila mtu anapenda Wi-Fi ya bure. Lakini unatakiwa kutambua kuwa taarifa (ikiwa ni pamoja na namba za kadi ya benki na nywila) zinazotumwa kupitia mitandao ya umma zinakuwa hazijasambulishwa (encrypted) na mtu yeyote kwenye mtandao huo anaweza kuzipata kwa urahisi.

Linapokuja swala la ununuzi unatakiwa kufikiria upya kufanya hivyo kwenye mitandao ya umma na badala ya chagua mitandao ya kibinafsi iliyo salama zaidi.

Tumia Nywila (Passwords) tofauti

Tunapenda kuwa wavivu linapokuja swala la kutengeneza nywila kwa ajili ya tovuti tofauti. Watu wengi wanachokifanya ni kutengeneza nenosiri na kulitumia kwenye akaunti zote wanazojiunga.

Hii ni hatari sana kwa sababu wakati hacker anaweka macho yake kwenye nenosiri la akaunti yako ya mtandao wa kijamii, basi anaweza kuchukua udhibiti wa taarifa zako za kifedha na kukuharibia.

Unda usernames mpya na nywila kila unapojiandikisha kwenye uanachama wa soko la mtandaoni.

Kwa upande wa nywila, ni muhimu kuzibadilisha mara kwa mara; angalau kila baada ya miezi sita. Changanya herufi ndogo na kubwa pia tumia na namba ili iwe vigumu kwa mtu mwingine kuzifikiria.

SOMA NA HII:  Je, Umewahi Kununua Simu Mtandaoni Ikaja Kwa Njia ya Posta na Ukaipata?

Mambo Mengine Muhimu

Hatua zingine ambazo unaweza kuzichukua ili kuwa salama unapofanya ununuzi wako mtandaoni ni pamoja na:

  • Usihifadhi PIN yako ya credit card kwenye kompyuta yako au maelezo yaliyoandikwa.
  •  Watu usio waamini usiwaambie nywila na logins zako.
  • Usiandike nywila na PINS wakati mtu mwingine anakuangalia.
  • Log out kwenye tovuti mara baada ya kumaliza ununuzi.
  •  Futa historia ya kivinjari (Clear browser history) kama unatumia kompyuta inayotumiwa na watu wengi.

Usikose sasisho zetu kuhusu vidokezo vya usalama kuhusu ununuzi mtandaoni.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA