Nyingine

Harmorapa ainunua bifu ya Diamond na Alikiba

Harmorapa aliyeteka vichwa vya habari kwa sasa nchini ameonekana kuanza kuununua ugomvi wa Diamond na Alikiba na kuzidi kuchafua hali ya hewa kwenye mitandao ya kijamii.

Harmorapa kupitia mtandao wa Instagram, amemtuhumu Diamond kuwa ndio aliyeanza kumchokoza Kiba hivyo anapaswa kumuomba msamaha. Kupitia mtandao huo hitmaker huyo wa Kiboko ya Mabishoo ameandika:

Mimi harmorapa mfalme wa bongoflaver and social network kwa sasa nasema kiukweli kutoka moyoni bwana mdogo #diamondplatnumz wewe ndo ulie anza kumrushia vijembe vya dharau Fundi #alikiba sasa usitafute suluhu kirahisi rahisi wewe platnumz nenda kwenye midia piga goti Muombe msamaa #alikiba kwani mkosefu ni wewe na sio #alikiba .
#now_naitwa_harmo_simba

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *