Sambaza:

Kampuni ya simu za mkononi ya Halotel imezindua huduma mpya ya kimasomo ijulikanayo kama ‘Halostudy’ itakayowawezesha wanafunzi nchini kusoma masomo yao kwa njia ya mtandao (TEHAMA).

Halostudy itakuwa ikipatikana kwenye simu za mkononi na kwenye kompyuta ambapo wanafunzi na walimu kote nchini watatumia bure, kitakachohitajika tu ni kuwa na internet kwenye simu zao au kwenye kompyuta zao.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Le Van Dai alisema kuwa, Halotel itandelea kushirikiana na serikali pamoja na wadau wengine wa elimu katika kufanikisha elimu inasonga mbele na kutengeneza wanafunzi bora wanaosoma masomo ya sayansi hasa kuelekea ukuaji wa uchumi wa viwanda.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) Dkt. Mussa Kisaka akizungumza jambo katika hafla hiyo.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo Cha Dar es Salaam Dkt. Mussa Kisaka alisema kuwa, mradi uliozinduliwa leo wa retooling ulihusisha mada za masomo zilizoonekana ngumu kufundisha na wanafunzi kujifunza hivyo kusababisha walimu wengi kukosa ujuzi wa masomo hayo na maarifa ya kufundishia. Hali hii imeendelea kupelekea wanafunzi wengi nchini kufeli masomo ya sayansi na hisabati,” alisema.

Aidha alisema kuwa, mradi huo ulihusisha Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kwa kutumia wataalamu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam uliweza kutengeneza maudhui ya mada zaidi ya 150 zilizokuwa ngumu na kuzifanya kuwa rahisi kufundishia.

SOMA NA HII:  Kenya yatengeneza satelaiti yake kurushwa anga za juu Machi mwaka huu

Hivyo basi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kiliwasiliana na wadau wa Halotel na walikubali kushirikiana na chuo hicho kuweza kumalizia mada zilizobaki na kuwapa nafasi wanafunzi wote nchini kuweza kufaidika .

Hivyo basi, kwa mwaka huu, Kampuni ya Simu ya Halotel, Taasisi ya Elimu (TEA) na walimu wa sekondari iliweza kumalizia mada zote zilizobaki sambamba na kuziweka kwenye mtandao kwa ajili ya wanafunzi kujifunza.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi aliipongeza kampuni hiyo kwa kufanikisha huduma hiyo itayowawezesha walimu wengi na wanafunzi kuingia katika mfumo mpya wa teknolojia nchini.

“Niwashukuru Halotel kwa kuendelea kuwa karibu na jamii. Nimefarijika kuzindua huduma hii ambayo naamini kabisa itawasaidia walimu na wanafunzi wengi katika kufanikia urahisi katika teknolojia,” alisema Hapi mbele ya wanafunzi na walimu waliohudhuria uzinduzi huo.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako