Hali ngumu ya kiuchumi imesababisha kampuni kubwa nchini kushuka mtaji DSE


HALI ngumu ya kiuchumi imesababisha ukubwa wa mtaji wa kampuni kubwa zilizoorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), kushuka kutoka Sh. trilioni 20.8 hadi kufikia SH. trilioni 20.4, anaandika Angel Willium.

kampuni kubwa
Ofisa Masoko wa DSE, Merry Kinabo

Akizungumza na waandishi jijini Dar es Salaam, Ofisa Masoko wa DSE, Merry Kinabo ameyasema hayo leo.

Alitaja kampuni hizo kuwa ni pamoja na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na Benki ya CRDB.

Ametaja sababu iliyochangia ukubwa wa mtaji wa kampuni hizo kushuka ni pamoja na kushuka kwa bei za hisa za KCB kwa asilimia 14, East Afrika Breweris Ltd (EABL) kwa asilimia 0.73 na National Media Group ( NMG) kwa asilimia 0.42.

SOMA NA HII:  M-Pesa na Tigo Pesa Zapokea Uthibitisho Kutoka GSMA

Kinabo amesema kampuni zilizoorodheshwa katika Soko la Hisa (DSEI), zimeshuka kwa point 38 yaani kutoka 2,162 hadi 2,124 kutokana na kushuka kwa bei za kampuni ya KCB.

“Yaliyojiri kwenye soko la hisa kwa wiki iliyoishia Ijumaa iliyopita Oktoba 13, mwaka huu ukubwa wa mtaji wa makapuni ya VODA, TBL na CRDB umeshuka kimtaji pamoja na soko la DSEI zimeshuka kwa point 38 kutoka 2,162 hadi 2,124,’’ amesema

Aidha, thamani ya mauzo ya hisa imepanda kutoka Sh. Bilioni 1.5 ya wiki iliyoisha tarehe 13 0ktoba 2017 hadi Sh. Bilioni 30 na idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imepanda kutoka hisa laki 6 kwa wiki iliyoisha Oktoba 13 2017 hadi hisa milioni 2.5 .

SOMA NA HII:  Netflix sasa ina wanachama milioni 125

Kampuni zilizoongoza kwa mauzo ya hisa ni kampuni ya VODA ,CRDB na TBL huku kampuni ya TSI ikipanda kwa point 11 kutoka point 3,814 hadi pointi 3,825 na kiashiria cha sekta ya viwanda (IA) kimepanda kutoka point 5,161 hadi 5,187.

Chanzo: Mwanahalisionline

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *