Intaneti

Google yapigwa faini ya dola bilioni 2.7 kwa kuzuia ushindani wa Kibiashara

Matangazo ya Google huoneka kwanza mtu anapotafuta

Google imepigwa faini ya ya dola bilioni 2.7 na tume ya ulaya baada ya tume hiyo kuamua kuwa Google ilikuwa imekiuka mamlaka yake ya kuweka matangazo yake binafasi kuwa ya kwanza.

Faini hiyo ndiyo kubwa zaidi iliyotolewa na tume ya ulaya hadi leo, kwa kampuni ambayo imelaumiwa kwa kukiuka sheria za biashara.

Amri hiyo pia inataka Google kundoa vizingiti vinavyozuia ushindani ndani ya kipindi cha siku 90 la sivyo ichukuliwe hatua zaidi. Kampuni hiyo ya Marekani inasema huenda ikakata rufaa.

Margrethe Vestager alisema kile ambacho Google imekifanya na haramu chini ya sheria za EU

Tume ya Ulaya ilisema inaiachia Google jukumu la kuamua ni mabadiliko yapi itafanyia mifumo yake ya mauzo.

“Kile ambacho Google imekifanya na haramu chini ya sheria za EU,” alisema Margrethe Vestager, kamishina wa ushindanii wa kibiashara wa tume ya EU.

Tume ya Ulaya imekuwa ikichunguza mifumo ya biashara ya Google tangu mwaka 2010.

Uchunguzi huo ulianza kufuatia malalamiko kutoka makampuni kama Microsoft miongoni mwa mengine.

Hata hivyo Microsoft hajatoa tamko lolote kufuatia uamuzi huo baada ya mahasimu hao kufikia makubaliano ya kujaribu kuzuia kesi mahakamani siku za usoni.

SOMA NA HII:  Facebook imesai deal kubwa na Universal Music
Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako