Sambaza:

Kampuni kutoka nchini  Marekani ambayo miaka ya karibuni imejizolea umaarufu mkubwa kutokana na uwekezaji wake kwenye masuala ya teknolojia, Google imezindua app mpya ya kupiga simu za video.

Ikionekana kama mpinzani kwa Skype inayomilikiwa na Microsoft, Google Duo inamuwezesha mtumiaji wa simu za kisasa (smartphones), kupiga simu za video kwa watu tofauti bure.

Ni App nyepesi sana kutumia na haitumii kiasi kikubwa cha Memory ukilinganisha na app nyingine za simu za video kama Skype na IMO. Unaweza kupakua (download) app hii hapa au kupitia Playstore kwa kutafuta “Google Duo”.

Pia wamezindua app nyingine inayoitwa Allo, hii ni chatting application kama ilivyo Whatsapp lakini hii ipo kipekee kabisa na itakuwa mpinzani mkubwa wa Whatsapp.

Moja ya sifa kubwa ya hii app ni kupunguza muda wa ku type kwa kukupa smart reply. Mfano mtu akikikutumia picha ya mbwa, hii app ina uwezo wa kujua hiyo picha iliyotumwa ni kitu gani na inakupa reply za kuchagua kama nice dog, ugly dog etc.

Kitu kingine kizuri kuhusu Allo ni kuwa integrated (kuchanganywa) na Google Assistant. Hii ina maanisha kwamba ukiwa unatumia hii app na unataka ku search kitu kwenye google basi utaweza kufanya hapo hapo ukiwa ndani ya hiyo app.

Hii ni tofauti kabisa na apps nyingine kama Whatsapp ambazo inakubidi utoke kwenye whatsapp uende kwenye google search halafu urudi tena kwenye whatsapp.

SOMA NA HII:  Vanessa Mdee amezindua ‘app’ ya simu ya Vee Money


Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako