Simu

Google wanasema simu 11 zita-support Daydream VR mwishoni mwa 2017

Mwanzo tulisikia taarifa kuwa Google Daydream VR itasupport kikamilifu simu za Samsung Galaxy S8. Sasa mkurugenzi mtendaji wa Google, Sundar Pichai amesema siku za karibuni simu nyingi zaidi zitakuwa na uwezo wa kutumika na Daydream.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa simu 11 zitasupport Daydream kabla ya mwisho wa mwaka. Hiyo inamaanisha tutaona angalau nyongeza ya simu kadhaa ndani ya miezi michache ijayo.

Tunajua kuwa Google inafanya kazi ya kutengeneza toleo jipya la simu ya Pixel, kwa hivyo ni sahihi kusema kuwa simu hizi zitasupport Daydream platform. Wakati huo huo, Galaxy S8 na Galaxy S8 + zinapata sasisho(update) ya programu ili kuwezesha ufanyaji kazi na Daydream, wakati ASUS ZenFone AR, ZTE Axon 7, Huawei Mate 9 na Porsche Design Mate 9, Motorola na Pixel / Pixel XL tayari zinasupport jukwaa hilo.

Itakuwa inavutia kuona ni vifaa gani vipya vitapata kibali cha kuwezesha Daydream kabla ya mwisho wa mwaka. Ni mara ngapi unatumia Daydream headset? Je, ni kitu ambacho unatumia mara mara kwa mara?

SOMA NA HII:  Simu 15+ za adroid zinazouzwa kwa bei nafuu unaweza kununua Tanzania hivi sasa
Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

Toa Maoni Hapa:

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako