Intaneti

Google inajaribu Video kujicheza zenyewe kwenye utafutaji “Search”

on

Google inafanya jaribo la video kujicheza zenyewe kwenye matokeo yake ya utafutaji (search results), kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa hivi karibuni.

Google inajaribu Video kujicheza zenyewe kwenye utafutaji "Search"

Kurasa kadhaa za matokeo zimeanza kuonyesha video, ikiwa ni pamoja na matokeo ya utafutaji ya sinema (movies) zinazotoka karibuni.

Trailers za sinema mpya zilionekana karibu na matokeo ya Utafutaji wa Google upande wa kulia wa ukurasa, na kuanza kucheza moja kwa moja.

matokeo ya google

Google

“Tunajaribu mara kwa mara njia za kuboresha uzoefu wa Utafutaji kwa watumiaji wetu, lakini hatuna mipango ya kutangaza hivi karibuni,” Google iliiambia Engadget.

Google iliongeza kuwa inafanya majaribio na trailer za filamu kwa muda mfupi.

SOMA NA HII:  Tech!! Apps 8 Unazoweza Kuzitumia Kugeuza Windows Pc Kuwa Wi-fi Hotspot

SOMA NA HII: Google kuunganisha Play Music na YouTube Red kuwa huduma moja

Ningependa kusikia kutoka kwako, je unafikiri mpango wa google kuruhusu  video kujicheza zenyewe utaboresha huduma ya utafutaji ? niandikie hapo chini sehemu ya comment.

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa Mediahuru Kila Siku Kwa Sababu Tunaaminika Katika Teknolojia.

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published.