Google Uptime: Unahitaji programu ya Kuangalia Video za YouTube na Marafiki Zako?


Google ina programu mpya – uptime-ambayo wewe na marafiki zako mtaweza kutazama video moja ya YouTube kwa wakati mmoja. Uptime kimsingi hufanya uzoefu wa kutazama video za YouTube kuwa wa kikundi/pamoja zaidi, hata kwa watu ambao wapo mbali mbali.

Watumiaji wa uptime wanaweza:

  • Tafuta video za YouTube ili kushirikisha jumuiya.
  • Tazama video ambazo tayari zimeshirikishwa na jumuiya.
  • Tazama video ambazo watumiaji wengine wanaangalia muda huo, pamoja na video zilizotazamwa hapo awali.
  • Kufuata (follow) watumiaji wengine ndani ya programu.
  • Kushiriki katika kutoa maoni, kupenda video na kutumia emoji reactions.

Kwa sasa, Uptime inapatikana tu kwenye vifaa vya iOS na inapatikana kupitia iTunes App Store.

Sasa, hapa tatizo langu ni hili, kwa nini Google iliunda programu mpya wakati wangeweza kuunganisha vipengele vyote kwenye YouTube.

Katika utetezi wake Google wamesema, jaribio la Uptime linatoka kwenye Google’s Area 120, ambalo huwawezesha wafanyakazi wa Google wenye fikra za kijasiriamali kujaribu mawazo mapya.

Ndio, Bado sielewi

Swali kwako, je unahitaji programu mpya kama uptime ili kutazama video za YouTube na marafiki zako? Wakati unaweza tu kumshirikisha kuona skrini yako kwa kutumia Skype au kutumia WhatsApp call na kuangalia video hiyo ya YouTube pamoja.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA