Google na Samsung Kujiunga na Teknolojia Mpya ya Magari Yanayo Jiendesha


Google, Qualcomm, na Samsung ni miongoni mwa makampuni 80 ya teknolojia yanayojiunga kuendeleza Chip mpya ya chanzo cha wazi (open-source chip design) kwajili ya teknolojia mpya kama magari yanayo jiendesha yenyewe.

Kwa mujibu wa ripoti ya The Information, kampuni ya Western Digital na Nvidia pia zinapanga kutumia chip mpya kwenye baadhi ya bidhaa zao, huku kampuni ya Tesla ikiwa tayari imejiunga na RISC-V Foundation na ina mpango wa kutumia teknolojia hiyo.

Wakati kampuni ya Arm inayotengeneza Chip hizo imekuwa na matumaini ya kuleta low-power/high performance processors kwenye mifumo ya AI na magari yanayo jiendesha yenyewe, Kampuni ambayo imetengeneza processor ya ndani ya simu janja yako inaweza kuwa na wasiwasi kwamba miundo mbadala kama hii inaweza kuharibu mafanikio yake ya baadaye.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA