Maujanja

Google Play Protect: Jinsi ya Kulinda Simu Yako ya Android Dhidi ya Virus

Wote tunajua ulinzi kwenye simu yako ni kitu cha msingi sana, lakini kadri siku zinavyoenda ndivyo inavyo zidi kuwa ngumu zaidi kulinda simu yako hii inatokana na sababu mbalimbali ambazo zingine hatuwezi kuzuia kwa mfano pale unapo install programu kwenye simu yako.

Hivyo basi leo tutaenda kujifunza jinsi ya kulinda simu yako ya Android ili isiadhiriwe na virusi mbalimbali, njia hii ni bora sana na inafaa kwa watumiaji wa simu zote za Android zenye akaunti ya Google.

Basi moja kwa moja twende tukangalie somo letu la leo, somo hili linatokana na kampuni ya Google kuleta sehemu mpya ya Google Play Protect ambayo imetokana na baadhi ya programu za Android kusemekana kuleta Virusi kwenye simu za Android . Hivyo Google wametengeneza sehemu maalumu kwaajili ya kulinda simu yako ili isiadhiriwe na virusi kutoka kwenye baadhi ya programu.

Sasa ili kuwasha sehemu hiyo inakuitaji kufuata hatua hizi rahisi sana ambazo zitakusaidia sana kulinda simu yako. Hatua ya kwanza ingia kwenye *Settings* au tafuta programu iliyo andikwa *Google Setting* kwenye simu yako ya Android kisha tafuta mahali palipo andikwa *Security * kisha chagua *Google Play Protect * kisha bofya sehemu iliyo andikwa *Scan
device for security threats * baada ya hapo utakuwa umewasha sehemu hiyo ambayo itakuwa inalinda simu yako masaa yote unapo install programu yoyote.

SOMA NA HII:  Unakubali? Windows Kuzipita Android Tablets Ifikapo Mwishoni mwa 2017.

Mpaka hapo utakuwa umewezesha simu yako kuwa salama na kuzuia virusi vinavyotokana na programu mbalimbali, kumbuka ili kuwa salama zaidi usi– install programu kutoka sehemu nyingine nje ya soko la Play Store.

Chanzo :Google Play Protect

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.