Intaneti

Google kuunganisha Play Music na YouTube Red kuwa huduma moja

Mkuu wa idara ya muziki wa YouTube, Lyor Cohen, amesema kuwa Google inaweza kuunganisha huduma yake ya “Play Music” na YouTube Red, kwa mujibu wa The Verge.

Google inataka kuunganisha Play Music na YouTube Red kuwa huduma moja

Cohen alitoa taarifa hiyo wakati wa mjadala maalumu, ambapo alisema Google inahitaji kuunganisha huduma hizo mbili ili kusaidia kuelimisha watumiaji na kuleta washiriki wapya.

Cohen aliongeza kuwa alitaka kufanya kazi moja kwa moja na lebo za muziki na wamiliki wa hakimiliki.

Kufuatia ripoti hiyo, Google imetoa taarifa ifuatayo: “Muziki ni muhimu sana kwa Google na tunatathmini jinsi ya kuleta pamoja huduma zetu za muziki ili kutoa bidhaa bora zaidi kwa watumiaji wetu, washirika wa muziki, na wasanii. Hakuna kitakacho badilika kwa watumiaji kwa sasa na tutatoa taarifa kabla ya mabadiliko. ”

Ningependa kusikia kutoka kwako, je unazungumziaje mpango wa Google kuunganisha huduma ya Play Music na Youtube Red ? niandikie hapo chini sehemu ya comment.

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa Mediahuru Kila Siku Kwa Sababu Tunaaminika Katika Teknolojia.

SOMA NA HII:  Angalia Maswali 10 Yanayoongoza Kutafutwa Kwenye Google
Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.