Habari za Teknolojia

Google Na Washirika Watatu Wawekeza $100M Kuboresha Miundombinu ya Broadband barani Afrika

Google na washirika watatu katika mkakati huu wameweka nia ya kuwekeza $ milioni 100 katika mradi wa miundombinu ya broadband, mradi utafaidisha miji ya Afrika, kwa kuwa na uwezo wa haraka na wa kuaminika wa internet katika bomba.

Makao makuu ya Google Mountain View, California.

Makubaliano yalisainiwa na wawekezaji wanne, Google, moja ya kampuni binafsi zinazoaminika katika masuala ya ICT barani Afrika Convergence Partners, International Finance Corporation (IFC), na shirika la pili kwa ukubwa katika biashara nchini Japan, Mitsui & Co, kuandaa mkakati wa kuundwa chombo kipya kinachojulikana kama CSquared.

CSquared itafanya kazi kama kampuni ya kujitegemea na itakuwa na ofisi Nairobi, Kenya, kwa mujibu wa BusinessDailyAfrica.

Uwekezaji huu wa miundombinu ya ICT ni mpango ugani wa Mradi wa Project Link, mpango ambao kwa mara ya kwanza Google waliuzindua nchini Uganda miaka minne iliyopita ili kutoa local internet service providers (ISPs) na uwezo wa kupata miundombinu yenye ufanisi zaidi.

Google Link Project imekuwa na stori yenye mafanikio, kukiwa na zaidi ya 1,600km ya mitandao ya fiber ambayo hadi sasa tayari imewekwa ndani ya miji mitano katika nchi ya Uganda na Ghana, kuwezesha watoa huduma ya mtandao na mitandao ya simu kutoa huduma nyingi zaidi.

Wakati Project Link imeweza kuboresha miundombinu ya broadband nchini Uganda na Ghana mpaka hivi sasa, CSquared yenye uwekezaji wa $ 100 milioni inalenga kwenye kupanua huduma hizo katika nchi nyingine nyingi za Afrika, kwa mujibu wa VentureBeat.

SOMA NA HII:  TANESCO yaanzisha mfumo mpya wa kulipia Bill

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako