Google Maps sasa inaweza kukuambia wakati sahihi wa kusafiri


Google inaongeza kipengele kipya kwenye Google Maps ambacho hakitakuambia tu jinsi ya kufika mahali fulani au safari itachukua muda gani, lakini itakuambia wakati mzuri wa kuondoka.

Kipengele kipya kinapatikana tu kwa watumiaji wa Maps kwenye Android, na kitaonekana wakati unajaza uelekeo. Pamoja na kukuonyesha muda na umbali wa kawaida unaohesabiwa, grafu mpya itatokea, inayoonyesha muda halisi utakaotumia kwenye safari yako  (unaonyeshwa kwa rangi ya kijani, njano, au nyekundu ili kuonyesha hali ya sasa ya trafiki) na makadirio ya utatumia masaa mangapi kama safari yako itaanza nusu saa mapema zaidi na itachukua muda gani kama utaanza safari masaa machache yajayo.

Haipo sahihi sana. Kwa kuangalia mfano hapo juu, kwa mfano, inaniambia kuwa ingekuwa haraka zaidi kuondoka nusu saa mapema, lakini ni vigumu kusema ni muda kiasi gani utaokolewa. Bado, inaonekana kama kitu chenye manufaa wakati unapojaribu kupangilia safari yako ijayo.

Kipengele kipya cha makadirio ya muda kinaonekana kwa watumiaji wa Google Maps kwenye Android kwa sasa, ingawa hakuna taarifa ni lini kitapatikana kwa watumiaji wa iOS.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA