Google Sasa Kuzuia Matangazo Kupitia Kisakuzi Kipya cha Chrome


Siku za karibuni, Google ilitangaza kuwa inafanyia kazi kisakuzi kipya cha Chrome ambacho kitakuwa na uwezo wa kuzuia aina fulani ya matangazo. Sasa, kisakuzi hicho kipo tayari na kitaanza kutumika rasmi.

Matangazo ambayo yatazuiwa na kisakuzi hicho kipya cha Chrome ni kama yale matangazo ya pop up, matangazo yanayo toa sauti, matangazo yaliyozidi kwenye tovuti pamoja na matangazo mengine mengi ambayo hayajakidhi vigezo na mashari ya Coalition for Better Ads.

Matangazo yatakayo zuiwa na kisakuzi kipya cha Chrome

Hii ni habari mbaya kwa watu wenye tovuti ambazo zina matangazo ya aina hii, ukizingatia Google pia imeanzisha sehemu mpya ambayo itakuwa kwenye tovuti ya Google Search Console ambayo ni maalum kwa watu wenye tovuti, sehemu hii italazimisha tovuti kuangaliwa na Google kama tovuti ina kidhi vigezo na mashari ya utangazaji hii ikiwa pamoja na kuangalia vigezo na masharti ya Coalition for Better Ads.

Kiasakuzi cha Google Chrome ni moja kati ya visakuzi vinavyotumiwa na watu wengi zaidi, hivyo lazima sehemu hii mpya italeta mabadiliko makubwa kwenye matangazo ndani ya tovuti mbalimbali. Kwa taarifa zaidi kuhusu sehemu hiyo ya kuzuia matangazo itakavyo fanya kazi unaweza kusoma HAPA.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA