Google itahamasisha wafanyakazi 10,000 kuboresha video za YouTube


YouTube hivi karibuni imezidi kupambana kwa nguvu zote dhidi ya video zisizofaa na kushughulikia channels na video zinazo kiuka maadili. Mkuu wa YouTube Susan Wojcicki ameelezea jinsi jukwaa hilo linavyolenga kuweka macho zaidi kwenye video baada ya kujifunza kupitia mapambano ya hivi karibuni dhidi ya maudhui ya kikatili.

YouTube

Wojcicki anasema kampuni hiyo imeanza kuipa mafunzo algorithms yake ili kuboresha usalama wa watoto kwenye jukwaa hilo na kuwa bora katika kuchunguza hotuba za chuki. Ili kuwa na uwezo wa kuifundisha algorithms yake video gani inatakiwa kuondolewa na ambayo inaweza kubaki, inahitaji msaada wa watu wengi zaidi. Ndiyo sababu inalenga kuteua watu 10,000 kutoka Google kutazama maudhui ambayo yanaweza kukiuka sera zake.

YouTube inasema kuwa machine-learning algorithms yake imesaidia kupunguza asilimia 70 ya maudhui ya ukatili mkali ndani ya masaa nane ya kupakia. Kwa kufundisha taratibu hizi kufanya vivyo hivyo kwa aina nyingine za video, kama vile video vinazo walega watoto, jukwaa litakuwa na uwezo wa kufuta video kwa kasi zaidi kuliko ilivyo sasa.

[irp]

Mbali na kupata msaada wa wafanyakazi 10,000 wa Google, YouTube pia inakusudia kuzingatia vigezo vikali wakati wa kuamua ni channels gani zinazostahili kutangaza.

Kwa sasa, wamiliki wa channels youtube wanahitaji angalau views 10,000 ili kupata pesa za matangazo, lakini inaonekana kama jukwaa litapanua timu yake ya wakaguzi wa channels na video “kuhakikisha matangazo yanafanya kazi sehemu inayostahili.”

Hatimaye, YouTube imeahidi kuwa wazi zaidi. Mwaka 2018, itaanza kuchapisha ripoti zilizo na data kuhusu mtandao huo, pamoja na hatua inazochukua kuondoa video na maoni yoyote ambayo yanakiuka sera zake.

One Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

  1. sidhani kama ni sehemu sahihi kuandika hili ila nawapongeza sana Mediahuru kwa aina ya website mliyotengeneza maana tumeshazoea kuona blog za udaku tu ila ushauri wangu tuchambulieni na vitu vingine kama magari,vifaa vya ndani na vitu vingine kwa sababu ni tehama pia

ZINAZOHUSIANA