Simu za Mkononi

Google inakaribia kununua kampuni ya HTC

on

Google Alphabet Inc inakaribia kununua kitengo cha kuunda simu cha Taiwan HTC Corp., kwa mujibu wa mtu anayejua hali hiyo, hizi ni jitihada za kuimarisha biashara ya simu ya kampuni ya google.

Google inakaribia kununua kampuni ya HTC-mediahuru

HTC, imewahi kushika nafasi za juu kama waundaji wa simu wakubwa dunia, mkutano wa HTC unatarajiwa kufanyika siku ya Alhamisi, kwa mujibu wa tovuti ya teknolojia ya Venture Beat, ambayo ilionyesha nakala ya mwaliko. Hisa pia zitasimamishwa katika soko siku ya Septemba 21 kutokana na tangazo la kusubiri, kwa mujibu wa soko la hisa la Taiwan.

Uthibitishaji wa aina fulani wa makubaliano kati ya Google na HTC umekuwa ukizungumziwa kwa wiki kadhaa sasa. HTC imekuwa ikifanya kazi na mshauri na alikuwa amekwisha andaa mkakati wa kuleta mwekezaji mwenye tija, kuuza biashara yake ya simu au kugeuza kitengo hicho, Bloomberg ameripoti mwezi uliopita, kwa mujibu wa watu wanaojua jambo hilo.

SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Infinix Zero 5 bei na Sifa zake

Apple Daily iliripoti Jumatano kuwa Google itanunua operesheni ya kubuni simu ya HTC kwa kiasi cha dola ($ 330,000,000). Google itaendelea kutumia brand ya HTC na itachukua wahandisi 100 wa HTC, tovuti hiyo iliripoti.

Kwa kumiliki haki za utengenezaji, Google inaweza kuboresha mauzo ya smartphone yake mpya ya Pixel, mpango mkakati wa kampuni hiyo kueneza programu yake muhimu ya Android na kushindana zaidi na Apple Inc.

Jaribio la mwisho la Google katika umiliki wa smartphone liliishi kwa muda mfupi: baada ya kununua biashara ya simu ya mkononi ya Motorola kwa dola bilioni 12.5, Google iliiuza ndani ya miaka mitatu baadaye kwa Lenovo Group Ltd kwa bei nafuu zaidi.

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published.