Apps za SimuSimu za Mkononi

Google “GBoard Keyboard” sasa inakuwezesha kutumia Maps na YouTube ndani ya app

Google inaonyesha kuwa na app kwajili ya kazi zote muhimu za simu za Android, kwanzia “Keep kwajili ya kuchukua note, Pixel launcher na hata app ya keyboard. Bidhaa zote hizi zinajaribu kuwaleta wateja kwenye huduma za Google zinazoingiza fedha nyingi kama vile injini ya utafutaji na YouTube. Lengo hilo linabakia kuwa kweli hata katika sasisho la leo la programu ya Google Gboard Keyboard app.

Kibodi ya Gboard inakuja na kitufe cha ‘G’ ambacho kina kila huduma ya Google ndani yake. Ikiwa unataka kushirikisha eneo lako kwa rafiki, kitufe cha G kinaweza kukusaidia kutokana na ushirikiano wake na Google maps. Kutoka kwenye kibodi unaweza kushirikisha eneo lako bila ya kwenda na kurudi kati ya programu ya Ramani na ujumbe mfupi.

Urahisi huo ulioongezwa pia unaweza kushirikisha video. Kitufe cha ‘G’ kitakusaidia “kuangalia video” kutoka YouTube moja kwa moja kutoka ndani ya app ya kibodi. Unaweza kushirikisha video kwa urahisi na wale unayozungumza nao. Matokeo ya Utafutaji kutoka Google pia yanaruhusiwa.

Mbali na kuiunganisha YouTube, Maps na Google Search, sasisho pia limeleta lugha zingine mpya; Ni pamoja na Kiarabu, Kiebrania na Farsi.

Kwa hiyo sasa ni muda wa kutumia kibodi hii wakati bado ya moto. Sasisho tayari linapatikana kwenye Play store, ikiwa hujaipata, ipe siku kadhaa, wakati mwingine inachukua muda kufika upande mwingine wa bwawa.

SOMA NA HII:  Simu za zamani zilizovuma miaka ya 2000 - 2005
Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako