Habari za Teknolojia

Google AutoDraw App Inataka Kumleta Msanii Aliye Ndani Yako

Wangapi mnaufahamu wimbo huu wa Donald Lawrence?

 

Naam, Google pia wanaamini katika wimbo huo, lakini badala ya kumwona Mfalme, Google wanaona Msanii.

Katika jitihada za kurahisi maisha yako ya kila siku, Google imezindua AutoDraw, huduma inayotumia teknolojia inayokuja kwa kasi ya utashi wa kompyuta (AI ; Artificial Intelligence) kumsaidia mtumiaji kuchora kwa ufanisi zaidi. Teknolojia inayozipa vifaa vya elektroniki kama vile kompyuta na simu uwezo mkubwa wa kujifunza na kumsaidia mtumiaji wake imekuwa ikikua kwa kasi sana katika miaka hii, uwezo huo wa kiakili kwa vifaa vya kielektroniki kama kompyuta unatambulika kwa jina la Artificial Intelligence.

google autodraw

Unaweza kutumia huduma kwa kutembelea wavuti ya http://autodraw.com kwenye simu yako, kompyuta au tablet bonyeza “Start drawing” . Hapo, unaweza kuchagua kalamu ya Autodraw na kisha kuanza kuchora toleo lako la kitu chochote.

Google Autodraw itaanza kutambua ni kitu gani unataka kuchora na hivyo kukupatia mapendekezo ya michoro mbalimbali iliyochorwa kwa usahihi zaidi. Ukichagua basi mchoro wako unaboreshwa kwa kutumia mchoro kutoka mfumo wa AutoDraw.

Mfano: Kushoto, mchoro uliochorwa na mtumiaji. Kulia, mchoro uliopendekezwa kutumika na AutoDraw

Kama nilivyosema, ni kama Robot inayojaribu kufanya unachotaka kukifanya.

Ukimaliza unaweza kusambaza mtandaoni kwa wengine au unaweza ukadownload katika mfumo wa picha wa PNG.

Je una mtazamo gani juu ya huduma hii?

SOMA NA HII:  Baada ya Vodacom na Airtel sasa ni SportPesa na Tigo

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.