Apps za SimuIntaneti

Gmail Smart Reply sasa inasupport Kihispania

Wiki chache zilizopita, Google waliongeza kipengele cha Smart Reply kwenye Gmail ambacho kinakuwezesha kujibu barua pepe zako kwa kutumia moja kati ya misemo mitatu ambayo imechaguliwa kulingana na mtindo wako wa kuandika. Inafanya kazi kwa kushangaza, na badala ya kutuma moja kwa moja, hufungua skrini ya kuandika huku maandiko yakiwa tayari yameandikwa ili uweze kuhariri unavyotaka. Ni kipengele muhimu kwa majibu rahisi.

huduma ya gmail

Sasa Google imetangaza kwamba Smart Reply sasa inasupport Kihispania katika vifaa vya Android na iOS. Ingawa kipengele bado kina mapungufu mengi , ni jambo kubwa kuongeza lugha nyingine. Kumbuka kutujulisha mtazamo wako utakapotumia kipengele hiki !

SOMA NA HII:  Tech!! Apps 8 Unazoweza Kuzitumia Kugeuza Windows Pc Kuwa Wi-fi Hotspot
Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako