Sambaza:

Smart Reply ni kipengele katika Inbox ya Gmail na Allo ambacho kinakuonyesha majibu ya haraka ambayo unaweza kuyatumia kujibu barua pepe, yameundwa kwa kuchambua barua pepe ulitumiwa. Tofauti na majibu ya haraka yaliyotengenezwa kabla(pre-made quick responses), majibu yanayopendekezwa yanafaa na yapo katika mtindo wako wa kuandika.


Sasa unaposoma ujumbe kwenye Gmail, majibu matatu ya smart reply yatapendekezwa kwako. Mara baada ya kuyabonyeza, unaweza kuhariri kabla ya kutuma. Kadri unavyozidi kutumia kipengele hiki, ndivyo Smart Reply hujifunza na huandika kama wewe.

Kipengele hiki kinapatikana kwa watumiaji watumiaji wa Android na iOS kwa lugha ya Kiingereza, huku Kihispania itaongezwa siku chache zijazo. Jaribu kuitumia na tujulishe unafikiria nini kuhusu kipengele hiki! Na ikiwa unataka maelezo zaidi ya jinsi inavyofanya kazi, andika swali ama ujumbe wako kupitia sehemu ya maoni hapa chini.


Sambaza:
SOMA NA HII:  Vidokezo 8 rahisi jinsi ya kukuza tukio lako kwenye LinkedIn

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako