Format memory card, flash drive (Njia ya kuondoa virus kabisa)


Njia rahisi ya kuondoa virusi kutoka kwenye kifaa cha nje (external device) ni kuformat memory card au USB flash drive kwa kutumia SDformatter. SDformatter ni programu ya bure ya kuformat memory card, na pia ina formats USB flash drive.

format
Kwa kutumia Windows OS, unaweza format external device, lakini Windows haiformat kila kitu. Hii ndiyo sababu hata baada ya ku-format kifaa cha nje kwa kutumia windows, baadhi ya virusi kama shortcut virus haviwezi kuondolewa kwenye kifaa. Kila mtu anaweza kuwa tayari ameshawahi kukutana na tatizo hili. Kwa sababu, mara tu virusi zinapoingia kwenye memory card, haiwezekani kuondoa virusi hivyo.

Makala hii inatoa suluhisho rahisi kwa tatizo hili. Ni rahisi sana kuformat memory card na pen drive kwa kutumia SDformatter. Nina hakika kwamba baada ya kuformat kifaa chako na SDformatter virusi zitaondolewa kabisa kwenye flash drive.

Programu nyingi ziko kwajili ya kuformat memory card au Pendrive. . Lakini ni rahisi sana kutumia SDformatter; ndiyo sababu ninapendelea kutumia SDformatter. Unaweza kushusha programu kamili ya SDformatter kwenye tovuti yake rasmi.

1.Jinsi ya Kuformat memory card au USB flash drive kwa kutumia SDformatter

1.Download SDformatter na kisha install.

2.Unganisha external device (memory card au pen drive) kwenye kompyuta.

3.Fungua SDformatter.

4.Jina la kifaa chako linapaswa kuonekana kwenye sanduku la mstatili, lililo karibu na “Drive” (Katika screenshot iliyo hapo juu inaonyeshwa kama “H”). Lebo ya ukubwa na Volume lazima ionyeshwe, vinginevyo bonyeza alama ya mshale, ambayo iko kwenye sanduku la mstatili karibu na “Drive” na uchague kifaa chako.

  1. Bonyeza kwenye “Options.”

6.”Option Setting” window itafunguka.

7.Bonyeza alama ya chini ya mshale ambayo iko kwenye sanduku la mstatili karibu na “FORMAT TYPE” na chagua “FULL (Erase)”.

8.Bonyeza OK.

9.Kisha bonyeza kwenye format.

Sasa angalia device properties za kifaa chako. Eneo la kifaa chako ambalo halijatumika lazima liwe sawa na nafasi kamili. Kwa njia hii, unaweza kuformat memory card na pia Pendrive kwa kutumia SDformatter.

Ikiwa njia hii haijafanya kazi, unatakiwa kufuata njia inayofuata.

2.Tumia safe mode

Virusi havifanyi kazi kwenye safe mode. Kwa hiyo tumia kompyuta yako kwenye safe mode na kisha format memory card au pen drive kwa kutumia system size option au kutumia SDFormatter.

Ikiwa njia hii haijafanya kazi, tumia njia inayofuata.

3.Tumia Internet security

Download trial version ya internet security yoyote. Scan vifaa vyako kikamilifu na uondoe virusi. Sasa unaweza kuformat kifaa chako cha nje.

Natumaini utakuwa umeipenda makala yangu kuhusu jinsi ya kuformat memory card. Ikiwa umefaidika na makala yangu, naomba usambaze makala hii kwa marafiki zako.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *