Nyingine

Forbes imewataja watu 10 matajiri zaidi duniani, utajiri wa Trump washuka

Jarida linalofatilia maisha ya watu maarufu na mali zao “Forbes” limetoa list ya watu matajiri zaidi duniani, na wakati huu kuna mabadiliko makubwa ya watu waliofanikiwa kuingia kwenye Top 10.

Mwanzilishi wa Microsoft Bill Gates kwa mara nyingine anaongoza orodha ya jarida la Forbes ya watu tajiri zaidi duniani mwaka huu. Kwa mujibu wa jarida hilo, mali za Gates zimeongezeka hadi $86bn, kutoka $75bn.

Idadi ya mabilionea (wa dola) duniani imeongezeka kwa asilimia 13 na kufikia 2, 043.

Anafuatwa na Warren Buffett, aliyeongeza utajiri wake kwa $14.8bn hadi $75.6bn.

Rais wa Marekani Donald Trump, hata hivyoa meshuka nafasi 220 hadi 544 kwenye orodha hiyo ya matajiri na sasa ana mali ya $3.5bn pekee.

Mfanyabiashara wa mitandao Mark Zuckerberg ambaye ni mmiliki wa mitandao maarufu ya kijamii kama Facebook, Whatsapp na Instagram amepanda mpaka nafasi ya 5 mwaka huu.

FULL LIST ya matajiri wa dunia hii hapa.

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *