Firefox Send: Mozilla Waja na Njia Mpya ya Kutuma na Kupokea Mafaili


Kampuni ya Mozilla ambao ni wamiliki wa kivinjari cha Firefox, wamekuja na njia mpya ya kutuma na kupokea ma-faili ya aina mbalimbali kwa urahisi kabisa.

Sehemu hiyo ambayo ipo kwenye majaribio inakupa uwezo wa kutuma ma-faili yenye ukubwa wa hadi GB 1, utofauti wa sehemu hiyo ni kuwa utapewa nafasi ya kutuma ma-faili ambayo baadae yatafutika ndani ya masaa 24.

Huduma hiyo waliyoipa jina la Firefox Send ipo wazi kwa watumiaji wa vivinjari vya aina yeyote, sio lazima firefox unaweza kutumia Opera, UC Browser au Chrome.

Kuwezesha sehemu hiyo huna haja ya kuwa na kisakuzi cha Mozilla bali unachotakiwa kufanya ni kubofya link hapo chini kisha upload file lako kisha mtumie link mtu unaetaka apate file hilo ataweza kudownload file hilo kwa urahisi kabisa.

send.firefox.com

Njia hii kutoka kampuni ya mozilla ni salama sana na mafaili yote yanayotumwa kupitia sehemu hii yana kuwa encrypted hivyo huna haja ya kuwa na wasiwasi pale unapotaka kuitumia.

Je Unaionaje huduma hii ya Firefox Send ?

3 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA