Firefox kwajili ya iOS ina mfumo automatic wa kuzuia matangazo na maudhui


Mozilla imetoa toleo lake la hivi karibuni la Firefox kwajili ya iOS, ambalo lina mfumo wa moja kwa moja wa kuzuia matangazo na maudhui katika Utafutaji wa Binafsi (Private Browsing mode), pamoja na chaguo la ulinzi wa kufuatilia katika kuvinjari mara kwa mara.

mediahuru

Kipengele hiki kinatumia teknolojia ya kuzuia matangazo katika Firefox Focus kwajili ya Android na iOS.

“Hatimaye tumeweza kuileta kwenye Firefox kwajili ya iOS shukrani kwa mabadiliko yaliyofanywa na Apple ili kuwezesha chaguo la third-party browsers,” walisema Mozilla.

Firefox kwajili ya iOS pia imeboresha “syncing” kwa watumiaji, na “content syncing” kwenye desktop zao.

Kampuni hiyo ilitangaza kuwa imeboresha Focus kwajili ya Android, na tabo nyingi (multiple tabs) katika kuvinjari kwa faragha (private browsing).

“Tumefanya uzoefu wa kuvinjari wa faragha kuwa bora zaidi kwa kuongeza msaada wa multitasking.”

Watumiaji sasa wana uwezo wa kufungua kurasa nyingi kwa wakati mmoja na kubadilisha kati yao.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA