AppsSimu

Firefox Focus imetoa toleo jipya baada ya kufikisha download milioni 1

Kutokana na kiasi kikubwa cha taarifa kinachokusanywa kutoka kwetu siku hizi, ni sahihi kusema kuwa suala la faragha linachukuliwa kama jambo kubwa na muhimu kwa watu wengi hivi sasa. Ndiyo sababu “ad blockers” zinazidi kuwa maarufu, pamoja na programu zingine na vipanuzi (extensions) zenye malengo ya kuzuia kiasi cha taarifa ambazo zinakusanywa kwetu.

Hii pia imesababisha kuongezeka kwa watengenezaji(developers) kama vile Mozilla kutengeneza vivinjari vya mkononi vinavyolenga kuwa na faragha kama vile Firefox Focus iliyozinduliwa mwaka jana. Sasa toleo la Android la programu hii lililozinduliwa mwezi uliopita limeonekana kuwa maarufu kwa watumiaji.

Mozilla wamethibitisha kuwa ndani ya mwezi mmoja tangu uzinduzi wake, app imefikisha downloads milioni 1 kwenye Android peke yake.

Pamoja na taarifa hiyo, Mozilla pia wametangaza vipengele vipya vilivyoombwa na watumiaji wa programu/app hiyo. Hii ni pamoja na kuruhusu kuangalia video zikiwa skrini nzima, kuruhusu kupakua (downloads), na pia wameboresha notification actions.

Mabadiliko haya yanapatikana kwenye toleo la Android la programu hii, kwa hivyo watumiaji wa Android wanaweza kwenda kwenye Google Play Store ili kufurahia app hii. Hatuna uhakika ikiwa kuna mipango ya kufanya hivi kwa watumiaji wa iOS, lakini ikiwa unataka kivinjari kilicholenga faragha basi unaweza kuangalia kupitia iTunes App Store.

SOMA NA HII:  Programu ya Kuchati ya AIM Kufungwa Baada ya Miaka 20
Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.