Sambaza:

Shirikisho la soka duniani FIFA March 28, limetangaza kumfungia mechi 4, nahodha wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya FC Barcelona ya Hispania, Lionel Messi kwa kosa la kutoa maneno machafu kwa mwamuzi katika mchezo dhidi ya Chile,Machi 24.

Adhabu hiyo ya Lionel Messi inaambatana na faini ya pound 8100, hivyo kufuatia adhabu hiyo Lionel Messi sasa ameanza kuitumikia kwa kukosa game dhidi ya Bolivia leo iliyomalizika kwa Argentina kupoteza kwa goli 2-0.

Messi alionekana kukasirika katika mchezo huo dhidi ya Chile baada ya mwamuzi msaidizi Marcelo van Gasse kuinua kibendera akiashiria mchezaji huyo kumfanyia madhambi mpinzani. Messi alirusha mkono wake juu na kumbwatukia mwamuzi huyo kwa kusema ‘la concha de tu madre’, kwa tafsiri ya “f*** off, your mother’s ****’ . .
Baada ya mchezo kumalizika kwa Argentina kushinda 1-0 kwa goli la Lionel Messi, nahodha huyo alikataa kumpa mkono mwamuzi huyo msaidizi.


Sambaza:
SOMA NA HII:  Hali ni mbaya sana kwa tovuti za Pirates na wazee wa Torrent

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako