Habari za Teknolojia

‘Female Iron Man’ amekamatwa akijaribu kuingiza iPhones 102 nchini China kinyume cha sheria

on

Mwanamke mmoja nchini China amekamatwa na askari wa uhamiaji wa nchi hiyo akiwa na simu za iPhones 102 ambazo zimefungwa kwenye mwili wake akiwa anasafiri kutoka Hong Kong kwenda  China mainland, kwa mujibu wa  9to5Mac.

Mwanamke huyo amepewa jina la“female Iron Man” na vyombo vya habari vya nchi hiyo, Alikamatwa baada ya maofisa katika jimbo la Guangdong mjini Shenzhen kuwa na mashaka naye na kuamua  kumweka kando kwajili ya kumfanyia uchunguzi. Mwanamke huyo alikuwa amevaa mavazi yasiyo ya kawaida kwa hali ya hewa ya joto katika eneo hilo.

Baada ya kumkagua mwanamke huyo, walikuta ana simu za iPhone 102 na saa 15 za kisasa zaidi. Smartphones za iPhone zina bei nafuu zaidi Hong Kong kuliko ilivyo sehemu zingine za China, na kufanya biashara ya ulaghai iwe na faida sana.

SOMA NA HII:  Nafasi za ajira serikalini sasa kuwafikia wahitimu kwa simu ya mkononi

Thamani kamili ya simu 102 za iPhone 7 Plus nchini Marekani ni karibu $ 100,000 (223980000Tsh), Ingawa iPhones 102 inaweza kuonekana kama idadi kubwa ya simu, lakini tukirudi nyuma mwaka 2015 mwanaume mmoja alikamatwa akijaribu kuingiza iPhones 146.

Mwezi juni mwaka huu, mfanyakazi wa Samsung kutoka Korea Kusini alikamatwa kwa kuiba smartphones 8,474.

Picha kwa hisani ya : XMNN

Chanzo: 9to5Mac

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published.