Elimu

Fanya haya wewe kijana uliemaliza kidato cha nne na hujachaguliwa kujiunga na kidato cha tano.

Mada ya leo inakuhusu wewe kijana mwenye ndoto ya manikio kitaaluma na pengine umekata tamaa. Kuna maelfu ya vijana kama wewe waliofanya mitihani ya kidato cha nne na sita nao kama wewe hawakupata nafasi ya kuendelea na ngazi ya juu ya mawazo.

Leo hapa nataka nikudaidie wewe uliokosa kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano 2015/2016 lakini una sifa za kujiunga na kidato cha tano au zakukuwezesha kuendelea na mafunzo katika tasnia mbalimbali katika shule na vyuo vya umemaliza (serikali) nchini Tanzania.

Basi kama wewe au ndugu yako ni mmoja wapo fanya yafuatayo kwa kuangalia lipi linakufaa kwa sasa.

1. SUBIRI SECOND SELECTION (chaguo la pili)
Endapo bado una nia ya kwenda kidato cha tano na umefaulu vizuri,mara nyingi serikali yetu imekuwa sikivu katika kuhakikisha kuwa kila kijana aliefaulu anachaguliwa kujiunga kidato cha tano,huwa inatoa second selection kwa wanafunzi wenye sifa za kujiunga na kidato cha tano,kwa hiyo kama wewe GPA YAKO ni kuanzia 1.6 na unahamu na kidato cha tano tafadhali subiri utachaguliwa.

TANBIHI :usibweteke na kusubiri tu hizo second selection fanya yafuatayo kwani kidato cha TANO sio maisha , maisha ni popote pale,basi fanya yafuatayo;

2. APPLY UALIMU KUPITIA NACTE
Nacte inahusika na vyuo vya ualimu kwa ngazi ya diploma na kushuka chini, Kama una sifa zinazohitajika omba ualimu fasta.

SOMA NA HII:  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel yatoa mafunzo ya TEHAMA kwa walimu

3. APPLY KOZI ZA AFYA KUPITIA NACTE
Nacte inahusika na vyuo vya vya afya kama ilivyo kwa ualimu kwa ngazi ya diploma na kushuka chini, Kama una sifa zinazohitajika omba kozi za afya haraka.

4. OMBA VYUO VYA KILIMO NA MIFUGO
Wizara ya mifugo inahusika na vyuo vya vya kilimo na mifugo kwa ngazi ya diploma na kushuka chini, Kama una sifa zinazohitajika omba kozi za kilimo na mifugo haraka.

5.APPLY SPECIAL PROGRAMME UDOM

MWISHO:
Endapo utaufanyia kazi ushauri wangu nina imani kubwa malengo yako yatafanikiwa mbele kwa mbele. Nikutakia mafanikio.

Zinazohusiana

JIUNGE NA MAZUNGUMZO, TOA MAONI YAKO HAPA

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Lako