Tech Support

Faili iliyopakiwa inazidi maelekezo ya “upload_max_filesize” katika php.ini

Ikiwa unakutana na ujumbe huu wa hitilafu:

The uploaded file exceeds the upload_max_filesize directive in php.ini

Wakati wa kujaribu kupakia faili au Plugin au kitu chochote kwenye tovuti yako ya WordPress, NA unahost tovuti yako kupitia web host inayotumia cPanel kama hosting control panel (ndio inatumika zaidi kama hosting control panel labda kama kampuni ya hosting imetengeneza ya kwao wenyewe ), basi hizi ni hatua zinazopaswa kurekebisha tatizo lako.

SOMA NA HII:  Je natakiwa kumiliki website au blog ?
  1. Ingia kwenye cPanel hosting control panel yako.
  2. Juu katika sehemu ya utafutaji (search bar) andika: phpfaili-mediahuru
  3. Hii italeta matokeo ili uweze kupata moduli inayoitwa “Select PHP Version”. Bofya hiyo. (Kama huioni, angalia troubleshooting hapa chini).
  4. Kwenye upande wa kulia wa ukurasa kuna kiungo cha bluu (blue link) kinachojulikana kama, “Switch to PHP Options”.. Bofya hiyo.faili
  5. Shusha chini ya ukurasa karibu na chini ya orodha inaposema, “upload_max_filesize”. Kwenye upande wa kulia inapaswa kutoa idadi, kama 2. Bonyeza namba na utaweza kuibadilisha. Badilisha kuwa kile unachohitaji (unaweza kuangalia ukubwa wa faili unalotaka kupakia).faili
  6. Kisha bonyeza “Apply”.
  7. Kisha bofya kitufe cha “Save”.
  8. Ikiwa una Plugin ya caching iliyowekwa kwenye tovuti yako ya WordPress, unatakiwa kufuta cache. Hakuna madhara jaribu tu kupakia faili yako tena, lakini ikiwa haifanyi kazi, jaribu kufuta cache zako na ujaribu tena.

Troubleshooting

Ikiwa hatua za hapo juu hazikuonekana kama nilivyoelezea, basi angalia kwenye cPanel yako ambapo unaweza kubadilisha ni “Theme” na ubadilishe kuwa “paper_latern”. Kila mandhari ina mpangilio wake na hata vipengele.

Ni matumaini yangu maelezo haya yamekusaidia.
Toa maoni ikiwa imekusaidia au una maswali.

Mada zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako