Faida za Kufanya Partition Kwenye Harddisk ya Kompyuta


Diski kuu “Hard disk drive (HDD)” inaweza kugawanywa katika sehemu (partition) nyingi tofauti. Sehemu zote zinafanya kazi tofauti.

Kwa kutumia diski moja, unaweza gawanya maeneo ya kuhifadhi data katika mafungu mbalimbali (Partition)

Tunaponunua kompyuta mara nyingi tunakuta tayari hard disk imeshagawanywa mara 2 au zaidi kulingana na ujazo wa kihifadhi data hicho lakini je, umewahi kujiuliza kugawanya HardDisk kuna faida gani (partitioned)? Karibu uweze kujua.

SOMA NA HII:  Jinsi ya Kugawa Partition Kwenye Windows bila "Kuformat"

Nini maana ya ‘partitioning‘?

Hii inamaanisha kitendo cha kugawanya kifaa cha kuhifadhi data kwenye kompyuta yako kinawezesha kuigawanya hard disk ya kompyuta yako mara nyingi utakavyo kulingana na ujazo wa Hard disk lakini daima programu endeshaji hukaa kwenye Local disk C.

Umuhimu wa kugawanya kihifadhi data cha kompyuta

Zipo sababu nyingi ambazo hufanya watu wafanye partition kwenye kompyuta kabla ya kuweka programu endeshaji. Hizi hapa ni baadhi ya sababu kuu zinatufanya tuigawanye hard disk:

  • Kufanya data zako kuwa katika mpangilio mzuri.

Iwapo hard disk yako imegawanywa basi data zako zitakuwa katika mpangilio mzuri kwani mafaili yanayohusiana na OS pamoja na programu nyingine wezeshaji yatakuwa katika partition yake huku data nyingine zikiwa kwenye partition tofauti; yaani Local disk C, D na nyinginezo.

  •  Urahisi wa kufanya recovery.

Kihifadhi data kinapopata majanga na iwapo hard disk ya kompyuta yako ilikuwa imegawanywa basi itakuwa rahisi kupata (recover) data zako pindi pale kifaa hicho kitakapokuwa katika hali yake ya kawaida baada ya kutengenezwa. ‘Back up’ ya programu endeshaji yako hakikisha kwenye mipangilio (settings) huwa inahifadhiwa kwenye partition (uhifadhi) nyingine kama vile D.

  • Usalama wa data zako.

Hard disk ambayo imeshagawanywa data ambazo zinahifadhiwa humo huwa salama zaidi. Kumbuka kama umeigawanya basi local disk C utaitumia kwa ajili ya kutunza programu endeshaji na programu wezeshaji wakati local disk D ndio utahifadhi mafaili yako. Hivyo hata kama programu endeshaji ikaathirika iwe kwa virusi, umeme kupita mwingi/kidogo na kusababisha kompyuta kuzima ghafla, n.k bado utaweza badili programu endeshaji na bado ukafanikiwa kupata data zako zote zilizopo kwenye diski D.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA